tangazo

Saturday, August 25, 2012

Wahalifu wa Kichina wakamatwa Angola

Raia 37 wa Uchina wamerejeshwa nyumbani kutoka Angola, ambako walikamatwa kwa tuhuma za kufanya uhalifu dhidi ya Wachina wenzao.
Wahalifu wa Kichina wakiwasili kwao kutoka Angola
Uhalifu huo ni pamoja na utekaji nyara, kunyang'anya watu pesa, wizi kwa kutumia silaha, na kulazimisha wanawake wauze miili yao.

Kikosi maalumu cha polisi wa Uchina kilitumwa Angola kushirikiana na polisi wa huko dhidi ya magengi ya Wachina yaliomo Angola.

Wizara ya Uchina ya usalama inasema magengi 12 yalivunjwa.

Wizara hiyo ilisema hii ni mara ya kwanza kwa polisi wa Uchina kufanya msako mkubwa kama huo dhidi ya wahalifu wa Kichina katika bara la Afrika.

No comments:

Translate