tangazo

Monday, August 13, 2012

YANGA YAIPIKU SIMBA KWA MBUYU USAJILI

 
 
 
 
 
                               Mbuyu akitia dole gumba fomu za Yanga. Kulia Bin Kleb
 
 
                                        Mbuyu anajaza fomu za usajili Yanga
 
 
 
 
 
KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam imeifanyia kitu mbaya sana Simba SC ambacho hawataamini maisha yao yote.
Kitu gani hicho? Ni kumsajili Mbuyu Twite na kumrudisha kwenye uraia wake wa asili, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), badala ya Rwanda aliopewa wakati akicheza nchini humo na kumbadili jina pia.
Kwa kumbadili uraia, Yanga wamepata na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya mchezaji huyo, kutoka Shirikisho la Soka (DRC), wakati huo huo, Simba wanahangaika kupata ITC ya mchezaji huyo kutoka FERWAFA, Shirikisho la Soka la Rwanda.  
Yanga inamsajili Twite kama mchezaji kutoka St Eloi Lupopo, klabu ambayo aliichezea kabla ya kutua APR mwaka 2006 kwa pamoja na ndugu yake, Kabange. Lakini mchezo uliochezwa hapa ni kwamba, APR imemrudisha Mbuyu Lupopo akitoka kucheza kwao kwa mkopo, ambao sasa wanamuuza Yanga.
Habari za kiuchunguzi, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata zinasema kwamba, Simba ilimsaini beki huyo wa APR kupitia Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage, kwa dola za Kimarekani, 10,000, lakini Yanga baadaye wakampandia dau.
Habari zaidi zinasema, Yanga inamsajili pia na pacha wake Mbutu (pacha wa kuzaliwa kabisa), Kabange, kwa sababu wachezaji hao kawaida yao kucheza timu moja daima.
Huko nyuma, Yanga iliwahi kuifanyia tena Simba ‘umafia’ kama huu katika usajili wa wachezaji, Charles Boniface Mkwasa na Yussuf Ismail Bana, miaka ya 1980.
Simba ilimsaiji beki wa Pamba kama Yussuf Bana, lakini Yanga wakaingilia kati na kumsajili kwa jina la Yussuf Ismail Bana, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Tanzania (FAT, sasa Shirikisho, TFF), wakati huo Said Hamad El Maamry akamuidhinisha beki huyo kucheza Yanga.
Simba walijaribu kumuiba kiungo Charles Boniface, aliyesajiliwa Yanga kutoka Tumbaku ya Morogoro na kumsajili, lakini baadaye Yanga wakamsajili pia na kumbadili jina, wakimpa Charles Boniface Mkwasa.
Mkwasa alifungiwa na FAT ya El Maamry kabla ya kufunguliwa baadaye na kuendelea kukipiga Yanga.
mshuwa.blogspot.com 

No comments:

Translate