tangazo

Thursday, August 23, 2012

HIVI ULIISIKIA HII KAULI YA CCM BAADA YA DR KAFUMU KUVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA.

                                                   Dr Dalaly Kafumu.

 Nafahamu kwenye vyombo vingi vya habari stori iliyochukua nafasi kubwa sana ni pamoja na hukumu iliyotolewa na mahakama iliyomuondoa kwenye ubunge aliekua mbunge wa jimbo la Igunga Dokta Dalaly Peter Kafumu.

Sasa stori mpya kuhusu hiyo hukumu imetoka kwa chama cha mapinduzi kwenyewe ambacho kimetefakari hukumu hiyo na kimejiridhisha kufanya uamuzi wa kukata rufaa kwa sababu haijaridhishwa.

Nape Nnauye ambae ni katibu wa halmashauri kuu ya CCM itikadi na uenezi amesema “tutakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama, hakuna kipya cha msingi ni kwamba tumeamua kukata rufaa, hatukuridhika na hoja zilizotumiwa na jaji kuutengua ushindi wa chama cha Mapinduzi na tunaamini kwenye rufaa tutashinda, hoja za Mahakama ni dhaifu sana”

No comments:

Translate