tangazo

Monday, August 27, 2012

RAGE AAHIDI KUMFIKISHA MAHAKAMANI TWITE AKIWASILI TANZANIA.

                                                              Mbuyu Twite.
 KLABU ya Simba kupitia kwa mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage imeweka wazi kuwa haijalipwa fedha za usajili ambazo ilimpatia beki Mbuyu Twite, ambapo imesisitiza kuwa iwe isiwe lazima walipwe fedha zao walizompa mchezaji huyo ikishindikana watafuata sheria zote ikiwemo kumfikisha mahakamani.

Rage amesema kuwa watafuata sheria zote za soka ambapo kuonyesha wamepania kufanya hivyo tayari wameshawakilisha pingamizi la mchezaji huyo kuichezea Yanga kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),

kisha ikishindikana wataenda katika mahakama za kiraia licha ya kuwa Shirikisho la Soka la Fifa haliruhusu masula ya soka kupelekwa huko.

“Tujafahamu kuwa Fifa hairuhusu masuala ya soka kupelekwa katika mahakama za kawaida, lakini alichokifanya Mbuyu ni criminal case, kwani alichukua fedha zetu kwa ajili ya kufanya kazi na sisi lakini hakufanya hivyo.

“Wao wanasema eti alikuwa na mkataba wa Lupopo, ulishaona wapi mkataba wa miaka sita! Nimefurahi Championi mmeeleza ukweli juu ya kila kitu kilivyokuwa kuwa, ni kweli tulimpa dola 30,000, lakini atatakiwa kutulipa jumla ya dola 39,500, zikiwemo za usumbufu na nauli tuliyompatia wakati anasaini mkataba wetu.

“Yanga hawajafanya haki katika hili, hatutakubali, wasipoturudishia fedha zetu akifika nchini tunamfikisha kwenye vyombo vya sheria, hatutakubali. Wawaulize TP Mazembe, nilisema nimewashika pabaya na kweli ilikuwa hivyo.

“Hivyo katika hili, Yanga nimewashika pabaya na wasilete ujanjaujanja,” alisema Rage.

No comments:

Translate