tangazo

Monday, July 30, 2012

MUME WA JACK ALILIA NDOA GEREZANI




THEA AANZA UPYA.



BAADA  ya mwigizaji Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’ kupata matatizo ya kupoteza kichanga chake juzikati, hivi ameanza upya kazi zake za uigizaji wa filamu.
Akizungumza na na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita jijini Dar, Thea alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kile kilichomtokea kwani yeye si wa kwanza kupatwa na matatizo hayo na sasa ameamua kurudi tena kwenye gemu.
Thea alisema kuwa ameamua kujichimbia kambini kwenye Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala, Dar kwa ajili ya kupoteza mawazo na kuanza kufanya shughuli zake kama ilivyokuwa mwanzo.
Mwanadada huyo ambaye ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’ alisema hapendi kuongelea kilichomtokea kwani anaamini siku ikifika Mungu atampa mtoto mwingine.

LULU APENYEZEWA CHAKULA CHENYE SUMU GEREZANI.





 LINGINE limeibuka! Kuna madai kwamba chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu kilipenyezwa kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam, mlengwa wa kukila alikuwa Elizabeth Michael ‘Lulu’, Ijumaa Wikienda limenasa data.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kijana kutoka Mwanza anayekadiriwa kuwa na miaka 18-20 anatajwa kuhusika na ubebaji wa chakula hicho ambacho hadi sasa haijajulikana nani amesimama nyuma ya zoezi hilo.
HABARI KAMILI
Habari zinasema kuwa siku chache zilizopita kijana huyo akiwa na mfuko wa rambo wenye chakula hicho alifika gerezani hapo na kufanya ujanja wa kuingia ili kumpa chakula Lulu.
“Huyu kijana alipofika hapa alitumia ujanja wake akaingia ndani kwa lengo la kumpa chakula Lulu akijifanya ametumwa na familia,” kilisema chanzo cha ndani.
Inadaiwa kabla hajafika kwenye eneo la kukutana na Lulu, maafande walio macho muda wote huku wakizingatia maadili ya kazi, walimnasa kijana na kumbana kwa maswali ambapo alishindwa kujibu na kuingia mitini.
“Kabla hajamfikia Lulu yule kijana alidakwa na maafande wa pale Segerea, akapigwa maswali, lakini baadaye akaingia mitini. Nadhani alijua kiwewaka. Hapo ndipo alipotiliwa shaka kuwa huenda chakula chake hakikuwa na usalama ndani yake na huenda kilikuwa na sumu,” kilisema chanzo hicho.
KINGEANGAMIZA WENGI
Kwa mujibu wa habari za ndani kutoka jeshi la magareza, raia anapotumikia kifungo kuna watu wake watatu tu, wenye picha za vipande (passport size) ndiyo wanaoruhusiwa kumpelekea chakula.
Sheria ya magereza inafafanua kwamba kabla mfungwa hajakula chakula alichopelekewa, mpelekaji anatakiwa kuwa mtu wa kwanza kukionja ili kuondoa shaka kama kitakuwa na kitu kibaya kwa hiyo kijana huyo angetakuwa kula kabla ya Lulu.
“Unajua yule kijana kama kweli alitumwa kumwingizia Lulu chakula chenye sumu, basi aliingizwa mkenge, maana kabla ya kumpa Lulu ale, angetakiwa kula yeye kwanza, sasa si angekufa!
“Mbaya zaidi, chakula hicho kingeendelea kutoa madhara kwa wengine maana kuna wafungwa huwa wanasaidiana chakula. Kwa hiyo unaweza kuona ni jinsi gani chakula kile kama kilikuwa na sumu kingeleta madhara makubwa,” kiliongeza chanzo.
NDUGU WAPONGEZA
Jumamosi (juzi) gazeti hili lilimsaka mama Lulu (Lucresia Karugila) kwa kupitia simu yake ya mkononi, hakupatikana lakini ndugu mmoja wa Lulu ambaye aliomba hifadhi ya jina alisema ndugu wamewapongeza maafande wa magereza ya Segerea kwa sababu walimudu vyema kumdhibiti kijana huyo.
Hata hivyo, ndugu huyo alisema hakuna ushahidi wa moja kwa moja kama kweli chakula hicho kilikuwa na sumu kwani wapo wanaoamini kuwa, kijana huyo ni shabiki mkubwa wa Lulu kwa hiyo aliamini kumpelekea chakula ni sehemu ya kutoa hisia za mapenzi yake.
KWA NINI KIWE NA SUMU?
Ndugu huyo aliendelea kudai kuwa sumu ilidhaniwa kuwepo kwa sababu toka Lulu ashikiliwe na vyombo vya sheria kwa madai ya kujua chochote kuhusu kifo cha Steven Kanumba, amekuwa akipewa ulinzi mkali kwa sababu ya mitazamo ya baadhi ya watu kwamba staa huyo ndiye aliyemuua Kanumba.

JESHI LA MAGEREZA LINASEMAJE?
Baada ya kupata taarifa hizo, Julai 24, mwaka huu waandishi wetu walifika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Tanzania, jijini Dar na kuzungumza na msemaji wa jeshi hilo, Omary Mtinga kwa lengo la kutaka kujua anasemaje kuhusu madai hayo.
Hata hivyo, msemaji huyo alisema jeshi lake halina taarifa hizo lakini akaomba apewe muda ili aweze kuzifuatilia.
Julai 28, mwaka huu, paparazi wetu alimpigia simu msemaji huyo na kumkumbushia kuhusu ahadi yake, lakini akasema yuko safarini nje ya jiji la Dar na alitarajia kurudi wiki inayoanzia leo.
Lakini kwa msisitizo mkubwa Afande mtinga alisema aliwatuma vijana wake wa makao makuu kufanya upelelezi mkali gerezani Segerea, kwa hiyo akirudi atapata jibu na kuyaweka wazi.
Akaongeza: “Lakini kama ni kweli ni kosa kubwa, mtu hawezi kupita bila utaratibu. Kila mfungwa ana utaratibu wa watu watatu kumpelekea chakula gerezani. Hata huyo (Lulu) ana watu maalum watatu wakiongozwa na mama yake mzazi ndiyo wanaoruhiswa kumpelekea chakula.”


Friday, July 27, 2012

SHEHE AZIFUMUA SWAUMU ZA MASTAA

                                                                       Rose Ndauka
                                                          Aunt Ezekiel
                                                                Frola Mvungi
                                                              Jacqueline Wolper


SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum amezifumua swaumu za baadhi ya mastaa ambao hufunga bila kufuata taratibu za dini ya Kiislam.
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum, Shehe huyo alisema funga ina taratibu zake hivyo mastaa wanaoingia kwenye ibada hiyo bila kuzifuata ni sawa na kushinda na njaa.
Alisema kitendo cha mastaa kufunga kisha baada ya kufungua kuendelea kufanya mambo yaliyo kinyume na Uislam ni sawa na kuoga kisha kuingia kwenye tope.
“Itakuwa ni jambo la ajabu kama utakuwa umefunga kisha kuendelea kuvaa vimini, kunywa pombe, kuzini au usiku unakwenda klabu. Wanaofanya hivyo ndani ya mwezi huu, ni sawa na kusema hawajafunga,” alisema shehe huyo.
Aidha, amewashauri mastaa Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper, Rose Ndauka na Flora Mvungi ambao katika siku za hivi karibuni walitangaza kusilimu kutobadilisha maamuzi yao kwani kufanya hivyo itakuwa ni kumcheza shere Mungu.
“Kwa hawa waliobadili nawasihi wasirudi nyuma na hata wakifunga wafuate maandiko yanasemaje, wasipofanya hivyo mwisho wao unaweza kuwa motoni,” alisema Shehe Musa.

MRISHO NGASA BADO ANAIPENDA YANGA.


Na Waandishi Wetu
WAKATI ikidaiwa kuwa majaliwa ya kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa kuwa shakani kwenye klabu yake ya Azam, hali ya mambo sasa inaonyesha ni kama filamu, kwani Ngassa ametamka wazi kuwa anaipenda klabu yake ya zamani ya Yanga ambayo imekuwa ikihusishwa kumsajili.
Ngassa ambaye aliifungia Azam bao la ushindi timu yake katika mechi ya nusu fainali Kombe la Kagame dhidi ya Vita Club ya DR Congo, jana kwenye Uwanja wa Taifa, aliwafuata mashabiki wa Yanga na kushangilia pamoja nao kisha baada ya mechi akarejea tena jukwaani hapo na kupewa jezi ya Yanga kisha kuivaa.
Ngassa aliyekuwa mchezaji pekee wa Azam akishangiliwa na mashabiki wa Yanga katika mchezo huo, baada ya mechi hakutoka uwanjani katika njia moja na wenzake badala yake alielekea kwenye lango lililokuwa na mashabiki wa Yanga ambapo ndipo alipopewa jezi hiyo na kuivaa.
Wakati huo wachezaji wenzake wa Azam FC tayari walikuwa wamerejea vyumbani huku wakisherekea. Baadaye Ngassa aliungana nao akiwa na jezi hiyo ya Yanga aliyoivaa juu ya jezi ya Azam.
“Naipenda Yanga kwa kuwa nimetoka nayo mbali, natamani kurudi ila naheshimu mkataba nilionao kwenye Azam, bao nililofunga limerejesha heshima yangu iliyopotea muda mrefu, kuna mengi yanayoendelea lakini huu siyo muda wake wa kuyazungumza,” alisema Ngassa.
Kumekuwa na taarifa kuwa Ngassa hana uhusiano mzuri na kocha wake katika klabu ya Azam, Stewart Hall na ndiyo maana amekuwa hampangi licha ya kuwa bado yupo kwenye kiwango cha juu.
Alipoulizwa juu ya hilo Hall alisema: “Ngassa ni mchezaji mzuri lakini anahitaji kujituma zaidi ili endelee kucheza kwenye kikosi cha kwanza.”
Mara kadhaa, Ngassa amekuwa akionekana makao makuu ya Yanga mitaa ya Jangwani na Twiga na ilielezwa ilichukua miezi kadhaa kabla ya kurejesha funguo za chumba alichokuwa akikitumia wakati akiwa Yanga.
Ngassa alijiunga na Azam FC kwa kitita cha Sh milioni 98 akitokea Yanga, hata hivyo ameshindwa kuonyesha cheche zake.

DIAMOND AMCHANA LIVE BABA YAKE MZAZI.

                                                             Baba mzazi wa Diamond(Abdull Juma)
                                                                       Naseeb Abdull(Diamond)



SIKU chache baada ya kuibuka kwa baba aliyemlea Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ aitwaye Abdul Juma na kudai kuwa mwanaye huyo amemtelekeza na hamjali, mwanamuziki huyo amemchana mzazi wake huyo, Ijumaa lina kitu kamili.

Akizungumza redioni kupitia Clouds FM, Jumatatu wiki hii, Diamond alidai kushangazwa na mzazi wake huyo huku akimtaka kuacha kusema maneno hayo kwani siyo mazuri.

Huyu hapa Diamond ambaye kwa sasa yupo juu kuliko msanii yeyote Bongo kimuziki:

“Kiukweli ni vitu ambavyo mimi vimenishangaza sana kwa sababu sijui chochote na nisingependa nisikie suala la mzazi wangu kusema mimi ni mtoto wake, sijui nini na nini kwamba mimi nafanya starehe sihusiki na yeye, siyo kauli nzuri kiukweli, ina maana ananijua kwamba mimi ni mwanaye baada ya kuwa Diamond?

“Siku zote kama alijua mimi ni mtoto wake, basi angenisomesha na kunipa elimu nzuri, lakini nilihangaika na mama yangu mzazi (Sanura Khassim ‘Sandra’) akanikuza na kunisomesha kwa shida na tabu zote mpaka leo nimekuwa hivi nilivyo, nisingependa kumsikia mtu yeyote anaongea kwamba mimi ni mtoto wake au yeye ni nani kwa sababu siku zote hawakuonekana, wasitake kuonekana kipindi cha masilahi, mtu ndiyo anajifanya anahusika sana na mimi kama mtoto wake.

“Haya mambo nilianza kuyasema toka nilipotoa single (wimbo) ya Binadamu, sikujua hata kama leo ningekuja kuwa na Prado (gari alilonunua juzikati la zaidi ya Sh. milioni 60), makazi (anajenga nyumba Tegeta, Dar na tayari imetumika Sh. milioni 69) au kuwa na haya mafanikio mengine, baba yangu ataendelea kuwa baba yangu tu ila siwezi kumpa kipaumbele kama ninachompa mama yangu kwa sababu kama angetaka hilo angenijali toka mapema.

“Mimi nilikuwa napenda kusoma na nilikuwa nafanya vizuri kwenye masomo yangu, lakini sikuwa na uwezo wa kifedha kuendelea kusoma, mzazi wangu alikuwa na fedha, ina maana angenijua mimi angenisomesha, leo ningekuja kuwa hata mbunge au waziri kwa sababu mimi najua nina upeo mkubwa sana wa kielimu na vitu vingine, sasa nimesota na muziki halafu leo ndiyo wanajitokeza.

“Sitaki, naomba waniache na mama yangu mzazi,” alitiririka Diamond.

TURUDI KWA MZEE ABDUL TENA
Baada ya kutoa maneno hayo makali kwa mzazi wake huyo, Ijumaa lilizungumza na mzee Abdul ambapo alisema kwa kifupi bila kufafanua: “Basi sawa siyo mwanangu.”

AKUMBUSHWA YA KANUMBA
Kwa mujibu wa mashabiki wa staa huyo mkubwa wa Bongo Fleva waliozungumza na Ijumaa juu ya sakata lake na baba huyo walimtahadharisha kwa kumkumbusha hali ilivyokuwa kwa marehemu Steven Charles

Kanumba ‘The Great’ na baba yake mzee Charles Kusekwa.
“Platnumz anatakiwa amalize suala hili kwa sababu nafikiri anakumbuka malumbano ya Kanumba na baba yake ambayo hayakuwa mazuri,” alisema Luda wa Kinondoni, shabiki namba moja wa Diamond.

TUJIKUMBUSHE
Wiki mbili zilizopita, mzee Abdul aliibuka na kuliambia gazeti ndugu la hili, Amani, kuwa Diamond ni mwanaye lakini hamjali na badala yake amekuwa akiponda starehe.

BADO UTATA
Hata hivyo, wiki moja baadaye ndugu wa Diamond waliibuka na kudai kuwa mzee Abdul siyo baba halisi wa msanii huyo bali baba halisi ni Idd Salum, ambaye alifariki mwaka 2004 ambapo Platnumz hakufafanua suala hilo.

MHE JOHN KOMBA AREJEA BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI INDIA

Kampteni Komba akiwa na mkewe, Salome Komba nyumbani kwako Kawe, jijini Dar es Salaam leo.


Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni mstaafu, John Komba amerejea kutoka India ambako amefanyiwa upasuaji kumtibu ugonjwa wa nyonga ulilokuwa ukimsumbua upande wa mguu wake wa kulia.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo, Julai 27, 2012, nyumbani kwake Mbezi, Kawe, Dar es Salaam, Komba alisema amerejea nchini, Juzi, baada ya kupatiwa matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad nchini India tangu mwanzoni mwa wezi huu.
Alisema, aliondoka nchini, Julai 2, 2012, baada ya kupelekwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu wa Bunge John Kashilila na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu hapa nchini kwa sababu ya mgomo wa madaktari.
"Siku napelekwa Muhimbili tu, tayari madaktari walikuwa wameanza siku ya kwanza ya mgomo wao, nikawa sina namna ila kuujulisha uongozi wa Bunge na kisha nikamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye kwa mamlaka yake akanisaidia haraka kama ambavyo huwasaidia wengine kwenda kutibiwa nje", alisema Komba.
Alisema, uzito ulichangia sana kusababisha mifupa kusagana kwenye nyonga upande wa mguu wa kulia, ambapo hadi anakwenda India alikuwa na uzindo wa kilo 138 wakati wastani wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana na ukumbwa wa mwili wake ni kilo 90 au 100 tu.
"Amesema, baada ya matibabu amerejea nchini akiwa na uzito wa kilo 128 ambao hata hivyo ametakiwa kuudhibiti na kuupunguza katika siku hizi ambazo atalazimika kupumzika nyumbani kabla ya kuanza kazi, Mwezi Septemba mwaka huu kama alivyoelekezwa na madaktari.
Akizungumzia upasuaji ulivyoendeshwa, Komba alisema, ulichukua saa tano na kukamilika bila matatizo katika upasuaji huo ambao alisema sehemu iliyopasuliwa ni ya ukumbwa wa futi moja.
Alisema, hata hivyo baada ya upasuaji huo, hakuweza kurejea katika wodi ya kawaida, kwa sababu majongwa kadhaa yaliibuka ikiwemo homa kali, presha, hivyo akalazimika kulazwa katika wodi ya wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) kwa siku tano.
"Sasa nimerejea nikiwa mzima, kwa sasa natumia fimbo hii, ili kuwezesha uzito uzilemee upande wa kulia nilikopanyiwa upasuaji, lakini sijambo kabisa", alisema Komba.
Komba alilaani baadhi ya vyombo vya habari ambavyo viliripoti kwamba katika kuugua kwake alikuwa mahututi na kwamba alikuwa anaugua figo.
"Jamani ninyi waandishi wa habari, jizoesheni kuandika habari zilizokamilika siyo kurashia-rashia tu na kuzusha uongo, mfano gazeti moja liliandika eti naugua figo nipo mahututi, wakati si kweli kabisa, ilikuwa jambo rahisi tu, kuja hapa nyumbani na kuniuliza au kuuliza mke wangu lingepata kwa uhakika ninachoumwa", alisema Komba.

Tuesday, July 24, 2012

Lucas Moura: Why the Brazilian Is Worth His Huge Transfer Fee for Man United



Sir Alex Ferguson is still looking for the next Cristiano Ronaldo.

No, Lucas Moura is not Cristiano; nor is Bebe. Cristiano wasn't the new George Best. But he was good enough.

When you are one of the greatest football managers the game has ever known, you have a right to covet the best players in the game.

When you have lived as long as Sir Alex—and have seen the talent he has seen, and managed some of it—then you are entitled to lust after the next great player.

Ronaldo was a game-changer. He was better than Besty in so many ways, but one thing they had in common was their selfishness. When they had the ball, they just wanted to run and score.

This is the one criticism that has been levelled at "Lucas" (as we shall call Lucas Moura, because everyone knows he's not Lucas Leiva).

He has many great qualities, but he can be selfish in the way that great players are, and that is sometimes resented by teammates.

Neymar has the same characteristic, and so did the previous great Ronaldo in his early years. Ronaldinho had it so badly that he wanted to show off all his tricks as well.

And that's when you ask yourself whether football takes itself too seriously?
Of course it's about money, because there is so much money at stake. West Ham and Southampton could get over £60 million in TV money this season.

That money can buy success (even if relative), and it can certainly buy survival. Which is why the Scottish teams that voted Rangers out of the SPL may be taking a long hard look at themselves at the end of the season—and at how many of them did not survive.

But George Best was a player that you would pay money to go and see. He could make the Old Trafford gasp with one touch, one feint, one dribble.

Cristiano Ronaldo had such qualities even as an 18-year-old when United played against Sporting Lisbon in the preseason of 2003.

At that time, he had played just 25 times for Sporting, but he had not played for his country. Lucas Moura has played 59 times for Sao Paolo at 19 and 15 times for Brazil.

Balozi Seif Idd Azungumza Na Wanahabari Kuhusu Kuzama Kwa Mv. Skagit


Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuunda Tume ya uchunguzi wa ajali ya Mv. Skagit iliyozama July 18 mwaka huu ambapo jumla ya abiria 290 walikuwemo katika meli hiyo.

Balozi Seif ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni kuhusiana na kuzama kwa meli hiyo.

Amesema Tume hiyo itaweza kuishauri Serikali nini cha kufanya katika kuhakikisha kuwa vyombo ambavyo vinachukuwa abiria vinakuwa vya aina gani na kuweka utaratibu mzuri utakaoweza kufanikisha usafiri wa baharini.

Ameongeza kuwa kutokana na hali ya ajali zinazotokea mbali na Tume hiyo,Serikali imeona kuwa ipo haja ya  kupitia sheria zinazohusu usafiri wa baharini na kuweka aina ya viwango vya meli zitakazoruhusiwa kuingizwa nchini na kuchukua abiria.

Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa nia ya Serikali juu ya ununuzi wa Meli kwa ajili ya usafiri ipo pale pale na kwamba juhudi zinaendelea katika kufanikisha suala hilo.

Akizungumzia kuhusu ajali hiyo Balozi amefahamisha kuwa jumla ya watu 146 mpaka sasa wameokolewa wakiwa hai ambapo Maiti 78 zilipatikana wakiwemo wanaume,wanawake na watoto.

Aidha amesema kuwa Chombo hicho kilikuwa na Raia wa kigeni 17 na waliookolewa wakiwa hai ni 15 mmoja amepatikana akiwa amefariki ambaye ni Raia wa Uholanzi na mmoja mpaka sasa hajapatikana.

Wageni hao kutoka nchi za nje ni wa Ubelgiji,Marekani,Ujerumani,Uholanzi pamoja na Israel na Serikali imetoa huduma kwa wageni hao na tayari wameondoka kurudi makwao kwa salama.

Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi alieleza kuwa kati ya majeruhi 138 waliopelekwa Hospitali kuu ya Mnazimmoja iliyopo mjini Zanzibar kwa uchunguzi hadi kufikia leo wagonjwa wote hao walikwisharuhusiwa baada ya kupata matibabu.
Amewataka wananchi popote pale ambapo wataiona maiti wapeleke taarifa kwa Jeshi la Polisi,Wakuu wa Wilaya,Mikoa na Masheha ili taratibu za kuihifadhi maiti hiyo ziweze kuchukuliwa.

Amesema kuwa zoezi la uokoji linaendelea na kuwashukuru wananchi Vikosi vya ulinzi vya Tanzania na vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na vyombo binafsi na wazamiaji kutoka nchi za nje kwa ushirikiano walioutoa uliofanikisha kwa kiasi fulani shughuli hiyo ya uopoaji wa maiti hizo.

KESI YA LULU YAPIGWA TENA KALENDA




KESI ya msanii wa fani ya filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu, imeahirishwa hadi Agosti 20 mwaka huu, kutokana na Jaji anayeisikiliza, DK Fauz Twaib, kuwa na majukumu mengine.Akiahirisha kesi hiyo jana, Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, alisema Jaji DkTwaibu, anakabiliwa na majukumu mengine.

“Jaji Twaib ni Mwenyekiti wa Baraza la Kodi na pia ni Mwalimu wa Sheria katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hivyo kwa sasa anatekeleza majukumu mengine katika nafasi hizo.Kwa hiyo kesi hiyo inaahirishwa hadi Agosti 20, mwaka huu,” alisema Msumi.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, yanayodaiwa kufanyika April 7 mwaka huu nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kesi hiyo ya msingi haijaanza kusikilizwa, tayari imeshafikia ngazi ya Mahakama ya Rufani, baada ya kuibuka kwa utata wa umri wa mshtakiwa huyo.

Utata huo uliiobuka baada ya mawakili wanaomtetea msanii huyo, kuomba kesi isikilizwe katika Mahakama ya Watoto kwa madai kuwa mteja wao bado ni mtoto kwa kuwa ana umri wa miaka 17 na si 18 kama, inavyoonyesha katika hati ya mashtaka. 

BASI LA TONY SLEY LAPATA AJALI LAUWA 3 LAJERUHI 38

                 
Hili ndilo basi la Tony Sley ambalo limepata ajali jana usiku na kuua watu watatu na kujeruhi 38
                  
                       Majeruhi wakisubiri matibabu Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Majeruhi wa basi la Tony Sley Bi Agnesy Lukasi akiwa na mtoto wake Dina Lukasi (4) wakisubiri kupewa matibabu katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kufikishwa hapo usiku huu wakitokea eneo la ajali mlima wa Kitonga
     
                Majeruhi wakipatiwa huduma Hospitali ya mkoa wa Iringa


Ajali ya basi ya Tony Sley yenye namba za usajili T 218 ACH lililokuwa likitokea Tunduma mkoani Mbeya kwenda jijini D’Salaam imeua watu watatu wakiwemo wawili raia ya Zambia na mmoja mtanzania na kujeruhi wengine 38.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la kona za mlima wa kitonga kwenye barabara kuu ya Iringa –D’Salaam jana majira ya saa 12 za jioni baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulipita lori lilolokuwa mbele yake.

Wakizungumza katika eneo hilo na Hospitali ya mkoa wa Iringa majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilolo Ilula walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wao alisema Agnes Lukasi (30).

Agnesy alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amekaa siti ya mbele na wakati dereva huyo akifanya uzembe huyo walikuwa wakimshuhudia hata kujaribu kumuonya bila mafanikio.

Alisema kuwa katika basi hilo alikuwa na mtoto wake Dina Lukas (4) ambaye pia amejeruhiwa katika paji lake la uso.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamhanda ambaye alifika eneo la tukio pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa aliuthibitishia mtandao huu kuwa jumla ya abiria 38 ndio waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

Aliwataja baadhi ya majeruhi ambao majina yao yamepatikana na kulazwa katika hospital teuli ya mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja na Boyd Simwings(43) , Violet Chambale(35),Zilombo Wake(38),Warmen Mambwe (33),Eugen Maluge(39), Mwamba Andrew (27) , Bright Mwalukanga (33) na John Lemba( 30) wote raia wa Zambia.

Wengine ni Martine Shombe( 29) mkazi wa Tunduma, Zainabu Amuri (32) mkazi wa D’Salaam , Efrain Mwampashi (31) mkazi wa Tunduma, Sebastian Mhaya(25) mkazi wa Tunduma, Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma, Mrashi Handu (38) mkazi wa Igulusi, Juma Ramadhan (40) mkazi wa Tunduma, Twaribu Juhim (39) mkazi wa Arusha, Muka Muka (26) mkazi wa Tunduma, Edina Ramadhan (3) mkazi wa Tunduma na Benjamin Enock (33) mkazi wa Mbeya.

Wengine ni Agness Lukas (30) mkazi wa Tunduma , Dina Lukas (4) mkazi wa Tunduma Beatrice Msakanti( 42) mkazi wa Zambia, Besa Shadrack (32) mkazi wa Zambia na Mary Mumba (48) mkazi wa Zambia pia.

Alisema majina ya majeruhi zaidi yatapatikana hivi karibuni baada ya majeruhi waliopo Hospital ya wilaya ya Kilolo Ilula kufika mjini Iringa.

Mbali ya majeruhi hao pia aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Cla Pily (32) na Dany Kawina (43) wote wafanyabiashara raia wa Zambia pamoja na Abel Nelson (32) ambaye ni mtanzania.

Kamanda Kamhanda mbali ya kueleza masikitiko yake juu ya ajali hiyo bado aliwaonya madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuendesha kwa uangalifu wa hali ya juu na kuwa jeshi lake mkoani Iringa halitalala kuwabana madereva wazembe.

Monday, July 23, 2012

Manchester United transfer target Lucas Moura given £40m price tag

Sao Paulo have set a £40million asking price for Manchester United and Chelsea transfer target Lucas Moura, after Real Madrid entered the race to sign the Brazil midfielder.

The 19-year-old is one of the hottest properties in South American football and has also been watched by
 scouts from Inter Milan, Paris Saint-Germain and Barcelona in recent months.
Lucas Moura is a target for Europe's biggest clubs (AFP/Getty Images) Lucas Moura is a target for Europe's biggest clubs   

Sao Paulo are determined to take advantage of the situation to maximise their return and, although they will not enforce the £65million buyout clause in Lucas's contract, they have made it clear they expect to receive a huge fee.

According to reports in Spain, Real Madrid sounded out the Brazilian club about a possible deal and were shocked to discover they valued the teenager at a minimum of £40million.

There is no reason for Sao Paulo to lower that price, as Lucas is under contract until 2015 and other clubs have expressed a firm interest.

The youngster's agent, Wagner Ribeiro, recently told Globo Esporte: 'Inter, Chelsea and Manchester United have already been in contact with me about him.'

Chelsea have the funds available to match the asking price, but it is likely to deter United, as it would require them to smash their transfer record.

Yanayohitaji kuzingatiwa kwenye katiba



Othman Masoud Othman ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar akitoa mada katika semina ya siku mbili kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kuhusu katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


 Kutokana na masharti hayo ya Katiba ni wazi kuwa Sheria zote za Mambo yote ya Muungano ambayo yameorodheshwa katika Jadweli la Kwanza (Mambo 37), Sheria zake zinapitishwa kwa utaratibu wa wingi wa kura. Kwa mfano, Sheria ya Uhamiaji, Sheria ya Uraia, Sheria ya Kuanzishwa kwa TRA, Sheria za kodi na Sheria zote za Muungano zinapitishwa Bungeni kwa wingi wa kura tu. Kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya Wabunge wa Zanzibar na Tanzania Bara, ni wazi kuwa Sheria za Mambo yote ya Muungano zinaamuliwa na upande mmoja tu wa Muungano.


MAMBO YA MSINGI KATIKA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA 1977
Muhtasari
1. JAMHURI YA MUUNGANO NA UTAIFA
2. MGAWANYO WA MAMLAKA
a. Mamlaka Tatu
i. Mamlaka ya Mambo ya Muungano
ii. Mamlaka ya Mambo yasiyo ya Muungano ya Zanzibar
iii. Mamlaka ya Mambo yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara
3. SERIKALI MBILI; MUUNDO WAKE
4. UENDESHAJI WA MAMLAKA TATU
a. Maamuzi ya Kisera
b. Utungaji Sheria
c. Usimamizi na Uendeshaji;
i. Fedha na Bajeti
ii. Utawala;
5. UTATUZI WA MIGOGORO YA MUUNGANO

SEHEMU YA PILI- UFAFANUZI NA MASUALI MUHIMU
JAMHURI YA MUUNGANO NA UTAIFA
Ibara ya 1 ya Katiba inatamka; “Tanzania ni Nchi Moja na ni Jamhuri ya Muungano…”
Ibara inaweka bayana kuwa Jamhuri ya Muungano ni Taifa moja lenye mfumo wa Jamhuri iliyoundwa kwa mfumo wa Muungano. Ibara hii imeandikwa sawa na vifungu vya Katiba vya nchi ambazo hazina Muungano kama vile Kenya, Uganda na Uturuki. Nchi nyingi zenye Muungano imara kama vile Switzerland na hata Urusi Katiba inaeleza bayana kuwa Taifa hilo ni Muungano wa Nchi au Washirika gani. Aidha hueleza hadhi ya Washirika hao ndani ya Muungano au Shirikisho hilo.
Masuali muhimu:

a. Kwa vile Taifa limeundwa kwa mfumo wa Muungano, je washirika wa Muungano huo ni wapi na ni wangapi;

b. Nini hatma ya washirika hao baada ya kuungana; wapo au hawapo tena (Angalia uhusiano wa suala hili Orodha ya Pili, Jadweli la Kwanza kuhusu kuendelea kuwepo kwa Sheria ya Muungano ya 1964 na pia Orodha ya Pili hasa vipengele vya 1,2 na 3);

c. Nini hadhi ya Washirika wa Muungano baada ya kuungana (Angalia mfano wa Katiba za Uswizi, Urusi, Marekani )

Kukosekana kwa ufafanuzi huu kumepelekea mkanganyiko mkubwa ndani ya Katiba kuhusu mipaka ya baadhi ya mambo. Mifano michache ni kama ifuatavyo:

a). Ibara ya 5 inayotoa haki ya kupiga kura utaofanyika Tanzania. Ibara hii inatoa picha kuwa ibara hiyo inatumika kwa uchaguzi wowote utaofanyika katika Jamhuri ya Muungano wakati ukweli ni kuwa Ibara hiyo inatumika kwa uchaguzi wa Muungano tu kwa Zanzibar .

b). Ibara ya 108 inaanzisha Mahkama Kuu ya Jamhuri ya Muungano. Kwanza hii inatafautiana na Ibara ya 4(2) ambayo inaeleza kuwepo Mahkama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Pili, Mahkama Kuu si miongoni mwa mambo ya Muungano na hivyo hakuna Mahkama Kuu ya Jamhuri ya Muungano; zipo Mahakama Kuu ya Zanzibar na Mahkama Kuu ya Tanzania Bara. Tatu, hili limepelekea kuchanganywa kwa Mahakama Kuu ya Tanzania Bara katika Uongozi wa Mahaka ya Rufaa jambo ambalo ni kinyume na Katiba na ni tofauti sana na mfumo uliokuwepo chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Mahkama ya Rufaa ya Afrika Mashariki haikuwa ya nchi yoyote bali ya nchi zote na ilikuwa na uongozi na bajeti yake tofauti. Aidha, mkanganyiko huu umepelekea mtafaruku katika uwakilishi wa Jamhuri ya Tanzania katika taasisi za kimataifa na kikanda kwa mambo yasiyo ya Muungano.
MGAWANYO WA MAMLAKA
Ibara ya 4(3) imegawa. Mamlaka tatu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka hizo ni kama zifuatavyo:
a). Mamlaka ya Mambo ya Muungano ambayo ni kwa Tanzania Bara na Zanzibar;
b). Mamlaka ya Mambo yasiyo ya Muungano kwa Zanzibar; na
c). Mambo yasiyo ya Muungano kwa Tanzania Bara
Mamlaka ya Mambo ya Muungano:
Kwa mujibu wa Ibara ya 4(3), Mambo ya Muungano ni yale yaliyotajwa katika Jadweli la Kwanza, mwishoni mwa Katiba. Kwa kawaida tumezoea kuyaita mambo hayo kuwa ni 22, lakini kwa uhakika ni haya yafuatayo:
i. Katiba ya Tanzania;
ii. Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
iii.Mambo ya nchi za Nje;
iv.Ulinzi;
v. Usalama;
vi.Polisi
vii.Hali ya Hatari;
viii.Uraia;
ix. Uhamiaji;
x. Mikopo;
xi. Biashara za Nje;
xii. Utumishi katika Serikali ya Muungano;
xiii.Kodi ya Mapato (income tax);
xiv.Ushuru wa Forodha (custom duty);
xv. Ushuru wa Bidhaa (excise duty);
xvi.Bandari;
xvii.Usafiri wa Anga;
xviii.Posta;
xix. Simu;
xx. Sarafu na Fedha;
xxi. Mabenki;
xxii.Fedha za Kigeni;
xxiii.Leseni za Viwanda;
xxiv.Takwimu za Viwanda;
xxv. Elimu ya Juu;
xxvi.Maliasili ya Mafuta;
xxvii.Mafuta yasiyochujwa;
xxviii.Gesi Asilia;
xxix. Aina Nyengine za Mafuta;
xxx. Baraza la Taifa la Mitihani;
xxxi. Usafiri wa Anga;
xxxii.Usafirishaji wa Anga;
xxxiii.Utafiti;
xxxiv.Utabiri wa Hali ya Hewa;
xxxv. Takwimu;
xxxvi.Mahkama ya Rufaani;
xxxviii.Uandikishaji na Mambo mengineyo yanayohusu Vyama vya Siasa.
Masuala Muhimu Kuhusu Mambo ya Muungano:
a. Idadi ya Mambo ya Muungano ni mangapi.
Suala hii linatokana na sababu tatu kubwa. Kwanza, kwa kuzingatia utaratibu wa kupiga kura chini ya ibara ya 98, jee mambo yaliopo chini ya Jadweli la Pili, Orodha ya Kwanza na ya Pili nayo ni mambo ya Muungano. Pili, Ofisi ya Rais na Makamo wa Rais hazikutajwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano, jee Ofisi hizo ni za Muungano au hapana. Tatu zipo Taasisi kama vile Tume ya Pamoja Ya Fedha hazikutajwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano. Nne, jee Serikali ya Muungano ambayo imetajwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano lakini ndiyo pia inayosimamia mambo ambayo si Muungano ni jambo kweli la Muungano. Tano, kwa mujibu wa Uamuzi wa Mahkama ya Rufaa katika Kesi ya Mchano Khamis na Wenzake 17, Orodha ya Mambo ya Muungano haikueleza mambo yote ya Muungano. Kwa hivyo, ni dhahiri kuwa Orodha halisi ya Mambo ya Muungano haijulikani.
b. Tafsiri ya Mambo ya Muungano
Si Katiba wala Sheria nyengine yoyote iliyotafsiri maana na mipaka ya mambo ya Muungano. Kwa mfano nini tafsiri ya elimu ya juu, Bandari, Aina nyengine za Mafuta zinajumuisha bio-fuels, Ulinzi nk.
c. Sera na Utaratibu wa Kubadili Mambo ya Muungano.
Mambo ya Muungano ndio msingi mkubwa wa Muungano. Kuongezwa au kupunguza mambo ya Muungano kunaweza kubadili dhana nzima ya Muungano. Hivyo kuwepo sera na utaratibu wa kubadili orodha ya Muungano ni muhimu sana. Kwa mfano Katiba ya Marekani inakataza kabisa Majimbo mawili kuungana kuunda Jimbo moja au Jimbo moja kugawanywa kuunda jimbo jengine, kwa sababu ya kulinda “utaifa” wa Majimbo. Katika Katiba ya Muungano kuna misingi gani ya Muungano ambayo.
d. Kukosekana Mfumo Rasmi wa Kila Mamlaka Kuitambua Mamlaka Nyengine
Hii ni kasoro kubwa sana katika Muungano na ambayo kwa bahati mbaya imejificha. Miongoni mwa athari zake ni kama zifuatazo. Kwanza, ingawa Rais wa Jamhuri ya Muungano ana mamlaka kwa mambo ya Muungano ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar, masuala kama vile ya Sheria za jinai si suala la Muungano na hivyo kinga aliyonayo ya kutoshtakiwa ndani ya Katiba ya Muungano haiwezi kutumika Zanzibar kwa vile Zanzibar ina mamlaka na sheria zake za jinai. Suala muhimu hapa ni jee Rais wa Muungano anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai ndani ya Zanzibar? Suala hili kwa hali ya sasa linaweza kuonekana la kituko, lakini ni la muhimu sana. Pili, suala kama hili ni muhimu kujiuliza kwa Rais wa Zanzibar anapokuwa ndani ya Tanzania Bara. Tatu, Katiba haijaweka bayana masuala ya mashirikiano ya kimahkama hasa katika utekelezaji wa amri za Mahkama za pande mbili. Jambo pekee lililoelezwa ni upelekaji hati za Mahkama. Yapo mambo mengi ambayo kwa sababu Katiba haijaweka bayana mfumo wa Mamlaka ya upande mmoja kuitambua Mamlaka ya upande mwengine, Taifa moja limebaki kama nchi tofauti sawa na nchi nyengine ya kigeni.
Mamlaka ya Mambo Yasiyo ya Muungano Zanzibar
Ibara ya 4(3) ya Katiba ya Muungano inaleta tafsiri kuwa mambo yote ambayo hayakutajwa katika Jadweli la Kwanza sio mambo ya Muungano. Ukiachia ibara hiyo hakuna kifungu chengine chchote cha Katiba wala Sheria kinachoeleza ni yapi mambo ambayo si ya Muungano. Hivyo, mamlaka ya mambo kwa Zanzibar inasimamia mambo yale ambayo hayakutajwa katika Orodha ya Mambo ya Muungano.
Mambo Yasiyo ya Muungano Tanzania Bara
Msingi wa mambo yasiyo ya Muungano kwa Tanzania Bara msingi wake pia ni Ibara ya 4(3) ya Katiba. Ufafanuzi zaidi utafanywa katika Sehemu ya Usimamizi wa mambo yasiyo ya Muungano.
SERIKALI MBILI NA MUUNDO WAKE
Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo kwa mujibu wa Ibara ya 4(2) ina dhamana ya kusimamia mambo ya Muungano na Mambo Yasiyo ya Muungano kwa Tanzania Bara, inaongozwa na Rais akisaidiwa na Makamo wa Rais! Waziri Mkuu na Mawaziri.
Kwa mujibu wa Ibara ya …. Rais huchaguliwa kwa wingi wa kura. Makamo wa Rais huchaguliwa kwa mtindo wa mgombea mwenza kwa fomula ya kuwa kama Rais atatoka Tanzania Bara, Makamo wa Rais atatoka Zanzibar na kinyume chake pia.
Waziri Mkuu, kwa mujibu wa Ibara ya 51(2), huteuliwa na Rais. Hakuna sharti la kikatiba wala kisheria linalomtaka Rais kushauriana na Makamo wa Rais katika uteuzi wa Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa Ibara ya 55(1) Ya Katiba, Mawaziri huteuliwa na Rais kwa kushauriana na WAZIRI MKUU sio MAKAMU WA RAIS. Rais wa Zanzibar ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri kwa wadhifa wake.
Hakuna ibara ya Katiba au kifungu cha Sheria kinacholazimisha Wizara za Serikali ya Muungano kuundwa kwa kuzingatia Wizara zinazosimamia mambo ya Muungano kutochanganywa na Wizara ambazo hazisimamii mambo ya Muungano.
Masuali Muhimu
a. Uhalali (legitimacy) wa Rais wa Muungano kuchaguliwa kwa wingi wa kura kwa kuzingatia tofauti ya idadi ya watu baina ya Zanzibar na Tanzania Bara;
b. Uhalali wa Rais wa Zanzibar kuwa Mjumbe tu wa Baraza la Mawaziri na sio Mwakilishi wa Zanzibar ndani ya Baraza la Mawaziri ili kuepuka kubanwa na Kanuni ya Baraza la Mawaziri ya Uwajibikaji wa pamoja
c. Nini wajibu wa kikatiba wa Makamo wa Rais katika uendeshaji wa Serikali;
d. Makamo wa Rais ni Msaidizi Mkuu wa Rais wa Muungano kuhusiana na Zanzibar kama ilivyokusudiwa na Mapatano ya Muungano? Jee ni Msaidizi Mkuu wa Rais wa Muungano kwa Mambo ya Muungano au Msaidizi Mkuu ni Waziri Mkuu?
e. Jee Mawaziri wanaotoka Zanzibar waliomo katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Muungano wanaiwakilisha Zanzibar au ni watumishi wa Rais wa Muungano kama walivyo Mawaziri wengine?
f. Jee kuna chombo chochote cha Kikatiba au kisheria kinacholazimisha Serikali mbili za Jamhuri ya Muungano kukutana, kushauriana na kufanya maamuzi ya pamoja kama Mamlaka mbili za kuendesha Jamhuri ya Muungano?
g. Katika mfumo wa sasa wa Serikali mbili upo uwezekano wa Serikali mbili zinazoongozwa na vyama viwili tofauti kufanya kazi kwa maelewano;
h. Jee kipo chombo cha kutatua mizozo inayoweza kujitokeza baina ya Serikali mbili?
USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA MAMLAKA TATU ZA JAMHURI YA MUUNGANO
a. Usimamizi na Uendeshaji wa Mambo ya Muungano
Katika kila eneo ni vyema tuangalie Usimamizi na Uendeshaji katika nyanja tatu;
Sera
Sera ndio dira ya maamuzi na utekelezaji wa jambo lolote la umma. Sera za Mambo ya Muungano zinaanzishwa na Wizara husika. Kwa mfano Sera ya Mambo ya Nje bila ya shaka itaanzishwa na Wizara ya Mambo ya Nje. Baada ya taratibu za ndani uamuzi wa mwisho hutolewa na Baraza la Mawaziri. Hakuna sharti la kikatiba wala la kisheria linaloitaka Serikali ya Muungano kushauriana na kukubaliana na Serikali ya Zanzibar katika kuandaa na kupitisha Sera za Mambo ya Muungano.
Utaratibu unaotumika kwa mazoea tu na kwa baadhi ya wakati ni rasimu za Sera kutumwa na Wizara husika kwa Wizara husika ya Zanzibar ili kupata maoni ya Zanzibar. Uzoefu wa siku nyingi unaonyesha Maoni hayo ya Zanzibar si mara nyingi kuzingatiwa. Mfano mzuri ni Sera ya Mambo ya Nje ambapo Baraza la Mapinduzi liliunda Kamati ya BLM kuandaa mapendekezo ya Zanzibar ambayo hatimaye yalipitishwa na BLM lakini hayakuzingatiwa.
Sheria
Kwa mujibu wa Ibara ya 64 mamlaka ya kutunga Sheria kwa Mambo ya Muungano ni ya Bunge.
Kwa mujibu wa Ibara ya 98, Bunge linapotunga Sheria linahitaji ridhaa ya Wabunge kutoka Zanzibar kwa Mambo yaliyomo katika Orodha ya Pili ya Jadweli la Pili. Mambo hayo ambayo ni 8 si sehemu ya Mambo ya Muungano ingawa baadhi yake ni mambo muhimu sana.
Kutokana na masharti hayo ya Katiba ni wazi kuwa Sheria zote za Mambo yote ya Muungano ambayo yameorodheshwa katika Jadweli la Kwanza (Mambo 37), Sheria zake zinapitishwa kwa utaratibu wa wingi wa kura. Kwa mfano, Sheria ya Uhamiaji, Sheria ya Uraia, Sheria ya Kuanzishwa kwa TRA, Sheria za kodi na Sheria zote za Muungano zinapitishwa Bungeni kwa wingi wa kura tu. Kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya Wabunge wa Zanzibar na Tanzania Bara, ni wazi kuwa Sheria za Mambo yote ya Muungano zinaamuliwa na upande mmoja tu wa Muungano.
Fedha na Bajeti
Ibara ya 133 ya Katiba ya Muungano inaanzisha Akaunti Maalumu ya Pamoja (Joint Finance Account). Ibara hiyo inaeleza wazi kwamba katika Akaunti hiyo, kutawekwa Mapato yote ya Muungano na Matumizi yote ya Muungano yatatoka katika Akaunti hiyo.
Ingawa Sheria ya Tume ya Pamoja ya Fedha ilipitishwa mwaka 1996, Tume ilianza kazi mwaka 2003 na kutoa Ripoti ya Mapendekezo ya kuanzisha Akaunti ya Fedha ya Pamoja na mfumo wa mgawanyo wa gharama na mapato ya Muungano mwaka 2006, bado Akaunti ya Pamoja haijaanzishwa. Suala kubwa hapa ni uhalali wa Bajeti ya Serikali ya Muungano kwa vile inakwenda kinyume na masharti ya Katiba ya Muungano.
Aidha, athari ya kutoanzishwa Akaunti ya Pamoja ni kama zifuatazo:
i) Mipaka ya Mambo ya Muungano haijulikani; kwa mfano, ingawa Bunge ni chombo kinachofanya kazi za Muungano lakini linafanya kazi kwa mambo yasiyo ya Muungano hivyo inahitajika kuweka uchambuzi wa kiasi gani ya gharama za Bunge zitoke katika Mapato ya Muungano na kiasi gani yatoke katika mapato yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara;
ii) Mapato ya Muungano hayawekwi bayana;
iii) Gharama za kuendesha shughuli za Muungano haziko bayana;
iv) Gharama za Mambo yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara hayako bayana. Aidha, haiku bayana ni kiasi gani cha mapato ya Muungano kinatumika kuendesha shughuli zisizo za Muungano kwa Tanzania Bara;
v) Stahiki au deni la kila upande kutokana na mapato na gharama za kuendesha shughuli za Muungano hazijaweza kuwekwa bayana.

Kwa madhumuni ya kujenga msingi mzuri wa Mjadala katika Mada hii sitazungumzia Uendeshaji na Usimamizi wa Mambo Yasiyo ya Muungano. Maelezo ya hapo juu yanatosha kueleza sehemu iliyobaki kuhusiana na Mambo yasiyo ya Muungano.
Utawala wa Mambo ya Muungano
Utawala wa mambo ya pamoja katika Muungano wowote ni jambo la msingi katika kuamua uimara wa

Muungano huo. Utawala wa mambo ya Muungano una sehemu mbili. Kwanza ni kuhusu ushiriki wa kila upande katika uongozi na ajira za mambo ya Muungano na pili ni pahala ambapo Ofisi za mamlaka husika ya jambo la Muungano yapo. Mambo hayo mawili ni muhimu sana kwa vile inasaidia kuleta sura ya Muungano, ujuzi kwa kila upande katika masuala ya Muungano na pia kupata faida ya uwekezaji wa Serikali ambayo ni ajira kwa raia.

Katika mfumo wa Muungano wa Tanzania hakuna sharti la kikatiba, la kisheria au sharti rasmi la kisera la Utawala wa Mambo ya Muungano.

Athari ya hali hii ni kuwa uongozi, ajira na uwekezaji katika Ofisi za mamlaka za Muungano zimekuwa upande mmoja wa Muungano.
Miongoni mwa mifano hiyo ni pamoja na:

 i) Makao Makuu ya Wizara zote;
ii) Makao Makuu ya Benki Kuu;
iii) Taasisi ya Kodi (TRA);
iv) Mamlaka ya Usafiri wa Anga;
v) Mamalaka ya Mawasiliano;
vi) Tume ya Pamoja ya Fedha;
vii) Uhamiaji;
viii) Tume ya Vyuo Vikuu;
ix) Mahkama ya Rufaa; na
x) Msajili wa Vyama vya Siasa

UTATUZI WA MIGOGORO
Chombo pekee kilichowekwa kutatua migogoro baina ya Serikali Mbili za Jamhuri ya Muungano ni Mahkama ya Katiba iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 125 ambayo taratibu zake zimeelezwa chini ya Ibara ya 126, 127 na 128. Mahkama hii kama chombo cha kutatua migogoro baina ya pande mbili ina kasoro kadhaa. Miongoni mwa kasoro hizo ni:

i) Ina mamlaka kuhusiana na mgogoro unaohusu tafsiri ya Katiba ya Muungano tu;
ii) Ni lazima ianzishwe kwa makubaliano ya pande zote mbili; kwa vile Majaji wake wanateuliwa kwa idadi sawa na Serikali mbili;

iii) Uamuzi ni kwa wingi wa kura;
iv) Inaundwa endapo patakuwa na shauri la mgogoro tu na si vyenginevyo.

HITIMISHO
Katiba ya Muungano ina maeneo mengi yanayohitaji kuangaliwa kwa makini. Hata hivyo maeneo yaliyofafanuliwa katika Makala hii ni miongoni mwa maeneo muhimu ambayo yanagusa nyanja takriban zote muhimu za Muungano.
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ZANZIBAR: OTHMAN MASOUD OTHMAN

WAZIRI HAMAD AJIUZURU.

 Mawaziri wanaohusika na usafiri baharini Zanzibar, Hamad wa kulia Dk Harison Mwakyembe na Said Ali Mbarouk waziri wa habari wakitoa taarifa kuhusiana na ajali ya meli juzi katika ukumbi wa ZBC Zanzibar

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake leo jioni imeelezwa. Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu  wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.

Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.
 “Tarehe  20 Julai,2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohammed Shein ya kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit iliyotokea Julai 18,2012” Ilisema taarifa ya Dk. Mzee.

Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dk Shein amemteua Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani(CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.
“Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,Rais amemteua Rashid Seif

Suleiman kuwa  Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano” Taarifa ya Ikulu ilisema.
Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano umeanza Julai 23 mwaka huu.

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni Meja Jenerali S.S. Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.

Hitma kwa waliokufa ajali ya meli leo

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(wa tano kushoto) pamja na Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Swala ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar,swala hiyo ikiongozwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) pamja na Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Hitma ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo
aadhi ya Waislamu waliohudhuria katika Hitma ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo
 
 
 
 
 
 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, leo ameungana na viongozi mbali mbali wa Kitaifa katika dua maalum ya hitma pamoja na Sala maalum ya Maiti (Salatul Mayyuit al-ghaib), iliyosomwa huko katika msikiti Mushawar, Mwembeshauri mjini Zanzibar. 
 Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT, iliyotokea hivi karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar-es-Salaam kuja Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa 


Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk. Amani Abeid Karume. 
 Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na wananchi na viongozi wengine.

Wabunge Wamsafishia Zitto Njia Ya Urais 2015

 
NI JOSHUA NASSARI WA CHADEMA, DEO FILIKUNJOMBE WA CCM, WASEMA KIGOMA WAJIANDAE KUTOA RAIS
Anthony Kayanda, Kigoma na Fred Azzah Dar
IKIWA imebaki miaka mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini mwaka 2015, wabunge wawili vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo.

Kauli za Wabunge hao zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea huku kukiwa na uwezekano wa umri wakugombea urais kushuka hivyo kuwawezesha wanasiasa wengi vijana akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo.

Wakizungumza katika tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma, Deo Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua Nasari wa Arumeru Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema), walisema wanaamini Rais wa 2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na ambaye ni mzaliwa wa mkoa huo.

Katika kauli yao hiyo, wabunge hao walisema Mbunge huyo ameonyesha umahiri mkubwa katika kusimamia mambo ya kitaifa bila upendeleo, jambo linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa hili.

Akimzungumzia kuhusu rais ajaye kutoka Kigoma, Filikunjombe alisema kundi la vijana lazima liungane kuhakikisha kuwa linatoa viongozi watakaopigania maslahi yao na Taifa kwa jumla ili kuleta ukombozi wa kifikra na kimaendeleo kwa maslahi ya jamii.

"Lazima mtambue kuwa, Tanzania ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba tunaweza kufanya makubwa katika kuleta maendeleo ya jamii katika nchi yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:

"Vijana wa Kigoma mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka michache ijayo lazima mkoa huu utoe Rais wa Tanzania."

Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini hapa kuhudhuria tamasha hilo lililopambwa na wasanii nyota wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma, Filikunjombe alisema; "Zitto anastahili kuwa rais".

Mbunge huyo wa CCM ambaye katika siku za karibuni ameonekana kuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa Zitto na Chadema, alisema Zitto anafaa kuwa Rais kwani amefanikiwa kuwaunganisha watu na kuleta umoja miongoni mwao, jambo ambalo linadumisha umoja wa kitaifa.

MENEJA WA MV SKAGIT AKAMATWA.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wamemsafirisha kutoka Dar es Salaam kumleta ZanzibarMeneja wa Meli ya Skagit Bw Omari Hassan Mnkonje(50) ili kuunganishwa na watuhumiwa wengine wanaohojiwa na Polisi visiwani hapa.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amesema kuwa meneja huyo wa ambaye ofisi zake zipo Jijini Dar es Salaam ameunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi hiyo.Meneja huyo alikuwa akishikiliwa na Polisi Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ataunganishwa pamoja na wenzake wengine waliokuwa wakihojiwa na Polisi Visiwani hapa.

Katika hatua nyingine Kamanda Ilembo amesema kuwa watuhumiwa watatu kati ya sita waliokuwa wakihojiwa kuhusiana na tukio hili wamewaachiliwa baada ya kuonekana kuwa hawahusiki katika tukio hilo.

Waliohojiwa na kuachiliwa huru ni pamoja na Fundi wa zamu wa meli hiyo Bw. Hamis Mbarouk Juma(60) ambaye naye alikuwa miongoni mwa manusura katika ajali hiyo.Wengine walioachiliwa baada ya mahojiano hayo ni Mtaalamu wa Vifaa katika meli hiyo Bw.
Ahmed Mashaka Mbarouk(51) mkazi wa Vikokotoni na Mhudumu wa Meli hiyo Bw. Shaibu Godfrey Francis Kanuti(33), mkazi wa Tombondo mjini Zanzibar.Watuhumiwa wanaoendelea kushikiliwa na Polisi liobaki katika kesi hiyo na ambao watafikishwa mahakamani siku za usoni Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara watakapokamilisha masuala ya mahojiano.Wakati huo huo, Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wanaoshiriki katika kazi ya utafutaji wa maiti leo wamefanikiwa kuzipata maiti nyingine watano na kufanya idadi ya maiti zilizopatikana hadi sasa kufikia 78.
Miongoni mwa maiti zilizoopolewa leo, moja imetambuliwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Kikosi cha Bendi Zanzibar STG Suleiman Pandu Jape.

Katika Maiti zilizopatikana leo, nne zilikuwa za wanaume akiwemo mtoto mdogo na mmoja ni ya mwanamke ambapo kufuatia kuharibika kwa miili hiyo, Kamishna wa Polisi zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuwa maiti hizozimefanyiwa mazishi katika makaburi ya pamoja yaliyopo eneo la Kama nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

MKUTANO WA CCM MJINI KIGOMA KATIKA PICHA.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI,) Aggrey Mwanri akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.
 Waziri wa Nchi Ofsi ya Rais, Mahusiano, Steven Wasira akihutubia kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tzeba akihutubia kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.
         Wazee kwenye mkutano wa CCM, Uwanja wa Community Centre Mwanga, Kigoma.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akituzwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba alipocharaza gitaa, kwenye mkutano wa CCM, Uwanja wa Community Centre, Mwanga Kigoma.
Habibu Ally wa kikundi cha Ujiji cha Sebene akicharaza kinanda akiwa chali wakati wa mkutano huo.

KIKOSI CHA YANGA SC KITAKACHOUMANA NA MAFUNZO MUDA MFUPI UJAO


1.Yaw Berko - 19,
2.Juma Abdul - 14,
3.Oscar Joshua - 4,
4.Nadir Haroub Cannavaro (C) - 23
5.Kelvin Yondani - 5
6.Athuman Idd Chuji - 24
7.Rashid Gumbo - 16
8.Haruna Niyonzima - 8
9.Said Bahanunzi - 11
10.Hamis Kiiza - 20
11.Stephano Mwasika - 3

Subs;
1.Ally Mustapaha 'Barthez' - 1
2.Godfrey Taita - 17
3.Ladislaus Mbogo - 29
4.Juma Seif Kijiko - 13
5.Idrisa Rashid - 12
6.Shamte Ally - 15
7.Jeryson Tegete - 10

Head Coach: Tom Saintfiet
Assistant Coach: Fred Felix Minziro,
Goalkeeper Coach: Mfaume Athumani
Team Physician: Dr Sufian Juma
Massagist: Jacob Onyango
Kit Manager: Mahmoud Omary (Mpogolo)

WOLPER, UWOYA WAPATANISHWA TENA LAIVU




TAKRIBANI siku 15 tangu wasanii Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyeinye’ na Jacqueline Wolper Masawe wapatanishwe na kumaliza tofauti zao, Ijumaa Wikienda linakuwa la kwanza kukujuza kuwa naye Irene Pancras Uwoya na Wolper wamepatanishwa.
Mchakato huo wa kumaliza tofauti na kuanza ukurasa mpya ulianza takribani miezi miwili iliyopita hadi Julai 18, mwaka huu, ulipofikia tamati pale Samaki-Samaki, Mlimani City jijini Dar es Salaam.

CHANZO CHA HABARI
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini kilichohusika na upatanisho huo, kilisema siku hiyo ya Jumatano wiki iliyopita, ndiyo ulikuwa mwisho wa mastaa hao wawili kutofautiana.
“Njoo fasta hapa Samaki-Samaki, yule Daudi Kipunguni mliyemwandika kanaswa na Sylvia Shally anawapatanisha Uwoya na Wolper.

IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya kumwagiwa ‘upupu’ huo, Ijumaa Wikienda lilitia timu Mlimani City lakini kutokana na foleni za jijini Dar halikuwakuta.
Baada ya kuwakosa, paparazi wetu alimwendea hewani shuhuda wa tukio hilo ambaye aliendelea kuthibitisha kuwa ni kweli wawili hao wamesuluhishwa.

SH. MILIONI 7 ZATUMIKA
Ijumaa Wikienda lilipododosa kuhusu mchakato huo ulianza lini na kama kuna gharama zozote zilizotumika, shushushu huyo alidai kuwa alimsikia Daudi (mpatanishi) akisema kuwa zoezi hilo lilichukua muda mrefu na kama ni suala la gharama siyo chini ya Sh. milioni 7.

WOLPER ANASEMAJE?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kuhusu ishu hiyo, mbali na kukiri kukutana na Uwoya Mlimani City, Wolper alifunguka kuwa walikutana mahali hapo kwa ajili ya chakula cha pamoja cha mchana.
“Tumemaliza tofauti zetu, sasa ni kazi tu ili kuelimisha jamii, mabifu hayana nafasi tena,” alisema Wolper.

UWOYA KAMA KAWA
Uwoya kama kawaida yake hakupatikana kwa kuwa siku hizi hana namba ya kumpata muda wote kwani zile za zamani zote hazipatikani.

WEMA ATIA NENO
Naye staa asiyechuja, Wema
Sepetu aliposikia upatanisho wa Wolper na Uwoya alikuwa na haya ya kusema:
“Sasa naamini mashabiki wetu watapata ladha yetu ambayo inawezekana waliipoteza siku nyingi, nimefurahi sana.”

KWANI TATIZO LILIKUWA NI NINI?
Miezi kadhaa Wolper na Uwoya waliingia kwenye vita nzito kisa kikiwa ni mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Ababuu ambaye alikuwa mchumba wa Wolper kabla ya baadaye kuwepo kwa tuhuma kuwa U

Translate