Wakuu wa Libya wanachagizwa kuchukua dhamana ya watu wanaokisiwa kuwa
5000, ambao wanazuwiliwa na makundi ya wanamgambo bila ya kufanyiwa
mashtaka rasmi.
Shirika la kutetea haki za kibinaadamu, Human Rights Watch, linasema
limeorodhesha kesi za watu ambao wameadhibiwa sana wakati wanazuwiliwa
na wapiganaji hao wa zamani.
Human Rights Watch inasema, wengi kati ya wale
wanaozuwiliwa ni wale waliokuwa wafuasi wa kiongozi wa zamani wa Libya,
Moammar Gaddafi, kabla ya kupinduliwa mwaka jana.
Wakuu wa Libya wakitakiwa wawe wameshapeleka kesi zote hizo mahakamani, ilipofika tarehe 12 Julai.
No comments:
Post a Comment