KESI
ya msanii wa fani ya filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu,
imeahirishwa hadi Agosti 20 mwaka huu, kutokana na Jaji anayeisikiliza,
DK Fauz Twaib, kuwa na majukumu mengine.Akiahirisha kesi hiyo jana,
Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam,
Amir Msumi, alisema Jaji DkTwaibu, anakabiliwa na majukumu mengine.
“Jaji
Twaib ni Mwenyekiti wa Baraza la Kodi na pia ni Mwalimu wa Sheria
katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hivyo kwa sasa
anatekeleza majukumu mengine katika nafasi hizo.Kwa hiyo kesi hiyo
inaahirishwa hadi Agosti 20, mwaka huu,” alisema Msumi.
Lulu
anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba,
yanayodaiwa kufanyika April 7 mwaka huu nyumbani kwa marehemu Sinza
Vatican, jijini Dar es Salaam.
Kabla
ya kesi hiyo ya msingi haijaanza kusikilizwa, tayari imeshafikia ngazi
ya Mahakama ya Rufani, baada ya kuibuka kwa utata wa umri wa mshtakiwa
huyo.
Utata
huo uliiobuka baada ya mawakili wanaomtetea msanii huyo, kuomba kesi
isikilizwe katika Mahakama ya Watoto kwa madai kuwa mteja wao bado ni
mtoto kwa kuwa ana umri wa miaka 17 na si 18 kama, inavyoonyesha katika
hati ya mashtaka.
No comments:
Post a Comment