Kando-kando ya mkutano wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika, AU,
marais wa Sudan na Sudan Kusini wamekutana kwa mara ya kwanza, tangu
nchi zao kukaribia vita awali mwaka huu.
Redio ya Sudan imeripoti kuwa Omar al-Bashir na Salva Kiir
walizungumza kwa saaa moja mjini Addis Ababa, na baadae walisema
wanataraji wataimarisha uhusiano baina ya nchi mbili zao - nchi
zinazozozana juu ya mpaka na mafuta.
Viongozi katika mkutano wa AU wamezisihi nchi
hizo zitatue ugomvi wao ifikapo tarehe mbili Agosti - muda uliowekwa na
Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment