Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(wa tano kushoto) pamja na Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Swala ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar,swala hiyo ikiongozwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) pamja na Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Hitma ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo aadhi ya Waislamu waliohudhuria katika Hitma ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein, leo ameungana na viongozi mbali mbali wa Kitaifa katika dua
maalum ya hitma pamoja na Sala maalum ya Maiti (Salatul Mayyuit
al-ghaib), iliyosomwa huko katika msikiti Mushawar, Mwembeshauri mjini
Zanzibar.
Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa
kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT, iliyotokea hivi
karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar-es-Salaam kuja
Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa
Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na Serikali
walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao wa
Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk.
Amani Abeid Karume.
Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar
Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la
Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe.
Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wawakilishi,
Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na wananchi na
viongozi wengine.
No comments:
Post a Comment