Mh mwakyembe.
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amefanya ziara ya
kushitukiza katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) na kusema, sekta
hiyo inakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu
zinazosimamia usafirishaji nchini.
Mwakyembe alifanya ziara ya
kushtukiza jana saa 11.00 alfajiri akitokea Dodoma anakohudhuria vikao
vya Bunge, kwa kile alichoeleza ni kuitikia wito kutoka kwa abiria
mmoja aliyempigia simu juzi usiku na kumweleza kuwa kunafanyika
ulanguzi wa nauli kwa abiria.
Katika ziara hiyo, Dk Mwakyembe
aliyeongozana na maofisa wakuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi
Kavu na Majini (Sumatra), Maofisa wa polisi wa Usalama barabarani,
aliamuru magari yaliyokuwa yamezidisha nauli kukamatwa na kutozwa faini
ya Sh250,000 pamoja na kuwarejeshea kiasi cha fedha kilichozidi abiria
wote.
“Ninachotaka mimi ni kila mtu kupata haki yake, wenye
magari fanyeni biashara kwa kufuata taratibu zilizopo. Katika ziara
yangu ya leo nimegundua katika sekta hii kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria
taratibu na kanuni zinazosimamia sekta hii na nitafuatilia ndani ya
kipindi cha miezi mitatu kuhakikisha tabia hiyo inakoma,” alisema
Mwakyembe.
Waziri huyo alitumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji
wa Sumatra ambao katika ziara hiyo waliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Ahmad Kilima kutumia nusu ya muda wao ndani ya ofisi na nusu inayobaki
nje ili kuhakikisha wanakamata magari yote yanayokiuka taratibu ikiwamo
la kuzidisha nauli kwa abiria.
Huku akipongezwa na abiria
waliokuwa wakielekea mikoani kwa kusaidia kurejeshwa kwa fedha zao, Dk
Mwakyembe alisisitiza kuwa vitendo vya ukiukwaji wa sheria kanuni na
taratibu zilizowekwa ikiwamo yaa kuzidisha nauli ni wizi na inawaumiza
wananchi ambao wengi wao ni masikini.
“Nauli kutoka Dar es
Salaam hadi Mwanza kwa basi la kawaida ni Sh45,000, kutoka Dar es Salaam
hadi Shinyanga Sh31,400 ni nani kati yenu amelipa zaidi? alihoji Dk
Mwakyembe akiwa ndani ya moja ya mabasi yaliyokuwa yanayofanya safari
za kutoka Dar es Slaam kwenda Mwanza. Kufuatia swali hilo, kundi la
abiria walisimama na kuanza kuonyesha tiketi zao ambapo Waziri huyo
aliamru konda wa gari hilo kuanza azi ya kurudisha fedha iliyozidi kwa
abiria wake kabla ya kuruhusiwa kuondoka katika kituo hicho.
Pia
Dk Mwakyembe aliamuru kila basi lililokutwa na kosa la kuzidisha nauli
pamoja na matatizo mengine kutozwa Sh250,000 kwa kila kosa na kusisitiza
kurudishwa kwa nauli za abiria.
Katika ziara hiyo, Dk Mwakyembe
aliwataja wamiliki kuwa wanachangia vitendo vya uvunjwaji wa sheria kwa
kushishindwa kuwawajibisha wafanyakazi wao pindi inapotokea malalamiko
kama hayo.
Waziri aliwataka madereva kutii sheria za barabarani
huku akisisitiza kwamba asimilia 75 ya ajali zinazotokea barabarani
zinatokana na uzembe wa madereva.
Kuhusu tatizo la madereva
kutokuwa na mikataba alisema atalifanyia kazi, lakini akataka nao
kuwasilisha malalamiko rasmi ofisini kwake ili aweze kuyafanyia kazi.
Adhabu kwa gari mbalimbali Makosa mbalimbali yaliyojitokea jana mbele
ya ukaguzi wa Waziri huyo wa uchukuzi ni makondakta kuzidisha nauli,
mabasi ya safari ndefu kuwa na dereva mmoja, baadhi ya mabasi kuwa na
leseni zilizokwisha muda wake na madereva kutokuwa na leseni.
Abiria waliozungumza na Mwananchi walipongeza hatua ya Dk Mwakyembe kuvalia njuga suala hilo wakisema hatua hiyo inaweza
kubadili tabia ya wafanya biashara kujihusha na vitendo vya ulanguzi wa nauli. Sumatra wanena
Kwa
upenda wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (Sumamtra) Kilima alisema
ukaguzi wa jana ulihusisha zaidi mabasi yanayofanya inazofanya safari
zake Dar es Salaam na Mwanza ambayo yalibainika kwa kiwango kikubwa
kujijihusha na vitendo vya kutoza nauli kupita kiasi.
No comments:
Post a Comment