BAADA ya mwigizaji Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’ kupata matatizo ya kupoteza kichanga chake juzikati, hivi ameanza upya kazi zake za uigizaji wa filamu.
Akizungumza na na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita jijini Dar, Thea alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kile kilichomtokea kwani yeye si wa kwanza kupatwa na matatizo hayo na sasa ameamua kurudi tena kwenye gemu.
Thea alisema kuwa ameamua kujichimbia kambini kwenye Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala, Dar kwa ajili ya kupoteza mawazo na kuanza kufanya shughuli zake kama ilivyokuwa mwanzo.
Mwanadada huyo ambaye ni mke wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’ alisema hapendi kuongelea kilichomtokea kwani anaamini siku ikifika Mungu atampa mtoto mwingine.
No comments:
Post a Comment