Bi Zena Mashaka
BINTI
mmoja mwenye ujauzito wa miezi nane, Zena Mashaka ,20, (pichani) mkazi
wa Urambo, Mkoa wa Tabora ametelekezwa na bosi wake katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili.
Taarifa zilizopatikana toka kwa wauguzi wa wadi
namba 38, hospitalini hapo zilidai kwamba Zena aliwaeleza kuwa alikua
mfanyakazi wa ndani kwa mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam ambaye
alimtoa kijijini na ameamua kumtelekeza Muhimbili akiwa mjamzito.
Wauguzi
hao waliomba wasitajwe gazetini walidai kwamba, Zena amekua akizungumza
vizuri lakini kuna wakati mwingine amekua akiongea mambo tofauti
inaonekana alipelekwa hapo akiwa ameshachanganyikiwa.
‘Unajua huyu
binti aliletwa hapa hospitali Juni 22, mwaka huu na mwanamke
aliyejitabulisha kwa jina la Zainabu Ali Saidi akifuatana na polisi wa
kike akidai kwamba walimkuta maeneo ya Kigamboni akiwa
amechanganyikiwa,” alisema muuguzi mmoja.
Muuguzi huyo amewashauri ndugu wanaomfahamu mgonjwa huyo kwenda kumuona wodini.
Afisa
Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Muhimbili, Mariana Kasili amethibitisha
kuwepo kwa binti huyo hospitalini hapo na amewataka ndugu wajitokeze
ili kumsaidia.
No comments:
Post a Comment