Rose Ndauka
Aunt Ezekiel
Frola Mvungi
Jacqueline Wolper
SHEHE
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum amezifumua swaumu za
baadhi ya mastaa ambao hufunga bila kufuata taratibu za dini ya Kiislam.
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum, Shehe huyo alisema funga
ina taratibu zake hivyo mastaa wanaoingia kwenye ibada hiyo bila
kuzifuata ni sawa na kushinda na njaa.
Alisema kitendo cha mastaa
kufunga kisha baada ya kufungua kuendelea kufanya mambo yaliyo kinyume
na Uislam ni sawa na kuoga kisha kuingia kwenye tope.
“Itakuwa ni
jambo la ajabu kama utakuwa umefunga kisha kuendelea kuvaa vimini,
kunywa pombe, kuzini au usiku unakwenda klabu. Wanaofanya hivyo ndani ya
mwezi huu, ni sawa na kusema hawajafunga,” alisema shehe huyo.
Aidha, amewashauri mastaa Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper, Rose Ndauka
na Flora Mvungi ambao katika siku za hivi karibuni walitangaza kusilimu
kutobadilisha maamuzi yao kwani kufanya hivyo itakuwa ni kumcheza shere
Mungu.
“Kwa hawa waliobadili nawasihi wasirudi nyuma na hata
wakifunga wafuate maandiko yanasemaje, wasipofanya hivyo mwisho wao
unaweza kuwa motoni,” alisema Shehe Musa.
No comments:
Post a Comment