tangazo

Friday, July 6, 2012

MWANACHUO WA CHUO CHA UALIMU ST. AGREY JIJINI MBEYA AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA BODABODA




                                           Pikipiki aliyotuhumiwa kuiba marehemu vedasto pius

                                         Vedasto pius akiwa amepoteza maisha baada ya kipigo
                                          Vedasto Pius baada ya kupigwa vibaya na wananchi




                                                        Kitambulisho cha marehemu vedasto pius



 Mwananchuo mmoja kutoka Chuo cha Ualimu cha ST Aggrey kilichopo Uyole jijini Mbeya, anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma za kuiba pikipiki ya kusafirishia abiria maarufu kama bodaboda.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30.

Mgonja amesema tukio hilo lilitokea mnamo Julai 2 mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika daraja lililopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara ya kuelekea Isanga, Jijini Mbeya.

Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada ya tuhuma za kuiba pikipiki yenye No T 438 BZU aina ya T-BETTER mali ya JOSEPH KAPASI (23) mkazi wa Ilomba jijini hapa.

Kwa upande wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae mtuhumiwa alipoanza kuendesha vizuri alitokomea na pikipiki hiyo. Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikutwa eneo la Isanga akielekea barabara ya Chunya akiwa na pikipiki hiyo ndipo alipoanza kupewa kipigo na wananchi wenye hasira kali mpka mauti kumfika.

No comments:

Translate