Zainuli Hassan
MTOTO
yatima Zainuli Hassan (16) (pichani) ambaye ni mwanafunzi aliyetakiwa
kuanza kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mbopo iliyopo Madale
jijini Dar es Salaam lakini ameshindwa kuanza masomo yake kutokana na
ukata, amepatwa na makubwa.
Zainuli alikuja katika ofisi zetu
akimwaga machozi akidai kuwa amefukuzwa katika nyumba aliyokuwa akilala
ambayo alisaidiwa kuishi. Katika toleo hilo tuliweka namba ya simu
ambayo ingewawezesha walioguswa na habari ile kuwasiliana naye hata
hivyo, amesema kuwa namba ya simu aliyotoa katika gazeti hili haikuweza
kupatikana kwa kuwa mwenye simu alimnyang’anya.
Ametoa namba
nyingine ambayo ni 0657 864 141 na bado anahitaji kusaidiwa ili aweze
kuanza shule. Tafadhali sana msaidieni kwani kutoa ni moyo- Mhariri.
No comments:
Post a Comment