tangazo

Thursday, July 12, 2012

BBC WALIHAMA JENGO LA BUSH HOUSE.

                                       Bush House,London maskani ya BBC kwa miaka 70

 Baada ya miaka 70 hatimaye Idhaa ya Dunia ya BBC imelihama jengo la Bush House.

 BBC haitapeperusha tena matangazo yake kutoka jengo hilo.

Taarifa ya habari ya mwisho toka jengo hilo ni majira ya saa 1200 saa za Uingereza.
Taarifa ya habari maalum kutoka kwa Mkurugenzi wa BBC, Mark Thompson ndio itahitimisha matangazo yote toka Bush House.

BBC ambayo ina peperusha matangazo yake kwa kwa lugha 28 inahamia hadi jengo lengine katikati ya mji wa London.

Shirika la BBC lilianza matangazo yake kwa lugha zisizo za kiingereza mwaka 1938 kutoka Broadcasting House eneo la Portland Place.

Lakini jengo hilo la awali lilipo shambuliwa kwa mabomu wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia ,ndipo BBC ikahamia Bush House mwaka wa 1941.

Na baada ya ujenzi mpya BBC inarudi tena maskani yake ya zamani ,Broadcasting House.
Wakati Bush House lilipofunguliwa mwaka wa 1925 lilikuwa ndilo jengo ghali zaidi. Enzi hizo ikikadiriwa kuwa la thamani ya Pauni milioni 2.

Bush House ambalo liko eneo la Strand mjini London, limeshuhudia matukio mengi ya kihistoria.
King George V mwaka wa 1932 alihutubia himaya yake yote kutoka jengo hilo. Nae Jenerali Charles de

Gaulle alitumia jengo hilo hilo kila siku kutuma ujumbe wa kuunga mkono vuguvugu la Free French movement baada ya kusambaratika kwa enzi za Nazi mwaka wa 1940 huko Ujerumani.

Hata hivyo BBC haikuwa mmiliki wa jengo hilo la Bush House ,bali mpangaja tu. Na wakati mkataba wake wa upangaji unapomalizika mwishoni mwa mwaka huu BBC itarejesha jengo hilo kwa wamiliki wake wa Kijapani.

No comments:

Translate