RVP arudi Ze Ganaz, Vidic kurudi Man United Msimu mpya!
RVP
Robin van Persie, ambae amechelewa
kurudi mazoezini kwa sababu alikuwa akishiriki Mashindano ya EURO 2012
na Nchi yake Holland, jana alirudi kujiunga na Arsenal lakini bado
kiwingu kimetanda kuhusu hatima yake kwa vile amekwisha tamka kuwa
hataongeza Makataba wake na Arsenal Mkataba ambao umebakisha Miezi 12
kumalizika.
Dalili za kung’oka Van Persie zimeanza
kuonekana baada ya Klabu ya Arsenal kutoitumia picha yake katika
kutangaza Jezi zao mpya kwa Msimu ujao kwenye Jarida lao la Mtandaoni.
Staa huyo kutoka Uholanzi anahusishwa na
kuhamia Klabu za Manchester City, Manchester United, Real Madrid na
hata Juventus lakini hadi sasa hamna kilicho wazi kama atabaki Emirates
au wapi atakwenda.
Hata hivyo, inategemewa uamuzi wa nini
hatima yake utajulikana kabla ya Jumamosi wakati Arsenal wanatarajiwa
kuondoka kwenda Kuala Lumpur, Malaysia ukiwa ni mwanzo wa Ziara yao
itakayowachukua hadi China na Hong Kong.
Vidic
Mechi ya kwanza ya Man United kwa ajili
ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England ni hapo Agosti 20 watakapokuwa ugenini
wakicheza Uwanjani Goodison Park na Everton.
Habari hizi njema kwa Wadau wa Man
United zimetolewa na Maneja wao Sir Alex Ferguson ambae pia
amethibitisha kuwa majeruhi mwingine, Chris Smalling, nae pia amepona
nyonga na ataonekana Uwanjani Msimu ukianza.
Hata hivyo, Sir Alex Ferguson amekiri
kuwa Beki wake mwingine Jony Evans, ambae alifanyiwa operesheni ya enka
yake, huenda asiwe fiti kwa ajili ya Msimu mpya.
Hivi sasa Manchester United wapo kwenye
Ziara huko Afrika Kusini na Jumatano Usiku watacheza Mechi na AmaZulu
Uwanja wa Moses Mabhida Mjini Durban ikiwa ni moja ya sherehe za
kuitukuza Mandela Dei, Siku ya kuzaliwa Shujaa Nelson Mandela ambae
anatimiza Miaka 94.
No comments:
Post a Comment