Kampteni Komba akiwa na mkewe, Salome Komba nyumbani kwako Kawe, jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
 wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga 
Magharibi, Kapteni mstaafu, John Komba amerejea kutoka India ambako 
amefanyiwa upasuaji kumtibu ugonjwa wa nyonga ulilokuwa ukimsumbua 
upande wa mguu wake wa kulia.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo, Julai 27, 2012, nyumbani 
kwake Mbezi, Kawe, Dar es Salaam, Komba alisema amerejea nchini, Juzi, 
baada ya kupatiwa matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo 
Hydrabad nchini India tangu mwanzoni mwa wezi huu.
Alisema, aliondoka nchini, Julai 2, 2012, baada ya kupelekwa na 
serikali kwa maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna 
Makinda na Katibu wa Bunge John Kashilila na kwamba alikwenda baada ya 
kukosa matibabu hapa nchini kwa sababu ya mgomo wa madaktari.
"Siku napelekwa Muhimbili tu, tayari madaktari walikuwa wameanza siku
 ya kwanza ya mgomo wao, nikawa sina namna ila kuujulisha uongozi wa 
Bunge na kisha nikamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye 
kwa mamlaka yake akanisaidia haraka kama ambavyo huwasaidia wengine 
kwenda kutibiwa nje", alisema Komba.
Alisema, uzito ulichangia sana kusababisha mifupa kusagana kwenye 
nyonga upande wa mguu wa kulia, ambapo hadi anakwenda India alikuwa na 
uzindo wa kilo 138 wakati wastani wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana
 na ukumbwa wa mwili wake ni kilo 90 au 100 tu.
"Amesema, baada ya matibabu amerejea nchini akiwa na uzito wa kilo 
128 ambao hata hivyo ametakiwa kuudhibiti na kuupunguza katika siku hizi
 ambazo atalazimika kupumzika nyumbani kabla ya kuanza kazi, Mwezi 
Septemba mwaka huu kama alivyoelekezwa na madaktari.
Akizungumzia upasuaji ulivyoendeshwa, Komba alisema, ulichukua saa 
tano na kukamilika bila matatizo katika upasuaji huo ambao alisema 
sehemu iliyopasuliwa ni ya ukumbwa wa futi moja.
Alisema, hata hivyo baada ya upasuaji huo, hakuweza kurejea katika 
wodi ya kawaida, kwa sababu majongwa kadhaa yaliibuka ikiwemo homa kali,
 presha, hivyo akalazimika kulazwa katika wodi ya wagonjwa waliopo 
kwenye uangalizi maalum (ICU) kwa siku tano.
"Sasa nimerejea nikiwa mzima, kwa sasa natumia fimbo hii, ili 
kuwezesha uzito uzilemee upande wa kulia nilikopanyiwa upasuaji, lakini 
sijambo kabisa", alisema Komba.
Komba alilaani baadhi ya vyombo vya habari ambavyo viliripoti kwamba 
katika kuugua kwake alikuwa mahututi na kwamba alikuwa anaugua figo.
"Jamani ninyi waandishi wa habari, jizoesheni kuandika habari 
zilizokamilika siyo kurashia-rashia tu na kuzusha uongo, mfano gazeti 
moja liliandika eti naugua figo nipo mahututi, wakati si kweli kabisa, 
ilikuwa jambo rahisi tu, kuja hapa nyumbani na kuniuliza au kuuliza mke 
wangu lingepata kwa uhakika ninachoumwa", alisema Komba.

 
No comments:
Post a Comment