Mv Seagul ikiwa Bandarini
Meli iliyokuwa imewabeba takriban watu miambili imethibitiswha kuzama
katika bahari ya hindi eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar. Meli hiyo kwa
jina SKAGIT ilikuwa inatoka Dar Es Salam kuelekea Zanzibar.
Kulingana na taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali.
Jeshi la polisi la wanamaji nchini Tanzania
limeanza shughuli za kuwaokoa watu zaidi ya mia mbili wanaohofiwa kuwa
kwenye meli ya Skagit inayoripotiwa kuzama huko visiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ingawa
hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini
wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali
katika eneo la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam
kuelekea visiwani Zanzibar.
Hadi hivi sasa vikosi vya uokoaji tayari vimeshapata maiti 12 kati ya maiti hizo 4 za watoto wadogo na maiti 8 za watu wazima wote ni raiya wa tanzania pia imeopolewa maiti ya mzungu ambaye hadi hivi sasa bado haijajulikana ni raia wa nchi gani.
Meli hiyo ilianza kupatwa na dholuba hilo muda mfupi baada ya kufika katika maeneo ya chumbe ndipo kepten wa meli hiyo alipowasiliana na idara ya usalama ili kuweza kuomba msaada juu ya tukio hilo.
Lakini hata baada ya kufika msaada huo ulikuta tayari meli hiyo imeshazama na kuwakuta baadhi ya abiria ambao walikuwa katika meli hiyo wakiwa juu ya mgongo wa meli hiyo.
Ila hali ni mbaya sana katika eneo hilo kwani kunamawimbi sana hadi inapelekea boti za uokowaji kushindwa kufanya vizuri kazi ya uokoaji,ila inavyoonekana ni watu wengi sana watakuwa wamepoteza maiza katika meli hiyo kwani hadi hivi sasa ni watu wachache sana wamepatikana wakiwa hai na wengi wao hawajulikani walipo.ila bado vikosi vya uokoaji vinaendele na shughuli hiyo
Tutaendelea kuwajuza kila tunapopata taarifa zaidi juu ya tukio hilo la kusikitisha.
No comments:
Post a Comment