Gari La Chegge ambalo amepata nalo ajali
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya, Said Nassoro ‘Chege’ amenusurika kifo baada
ya kutokea ajali ya gari aina ya Corona alilokuwa akiendesha, kumgonga
mwendesha pikipiki katika barabara ya Mbozi, Temeke jijini Dar es
Salaam, juzi usiku.
Chege ambaye pia ni memba wa kundi la TMK
Wanaume Family amesema kuwa licha ya kutokea kwa tukio hilo, hakupata
majeraha makubwa zaidi ya kupata mtikisiko katika bega lakini baada ya
muda afya yake ilitengemaa.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni miezi
miwili tangu kutokea kwa ajali iliyosababisha kifo cha aliyekuwa kiungo
wa Simba, Patrick Mafisango maeneo ya karibu na chuo cha Ufundi Stadi
(Veta), ikiwa ni mita chache kutoka sehemu ambayo Chege amepata ajali.
“Ajali imetokea jana (juzi) usiku majira ya saa tano, nilikuwa natoka
Sinza naelekea Temeke, ndipo ghafla ilitokea pikipiki iliyokuwa
ikiendeshwa kasi na jamaa ambaye baadaye ilibainika kuwa alikuwa
amelewa, ndipo tukakutana uso kwa uso, alivunjika mguu na majeraha
mengine.
“Gari limeharibika sana sehemu ya mbele imefumuka, lipo
Kituo cha Polisi cha Chang’ombe, pia kumbe jamaa alikuwa ameiba pikipiki
hiyo ndiyo maana alikuwa kwenye kasi kubwa, nimeondoka asubuhi (jana)
na sasa nipo Kigoma kwa ajili ya shoo ya Kigoma All Stars,” alisema
Chege ambaye ni mwenyeji wa Kigoma.
No comments:
Post a Comment