tangazo

Tuesday, July 17, 2012

TUZO YA UEFA MCHEZAJI BORA 2011/12


TUZO YA UEFA MCHEZAJI BORA 2011/12: Listi ya Wachezaji 32 yaanikwa!

MESSI_V_RONALDOLionel Messi, Mshindi wa kwanza wa Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora Ulaya kwa Msimu wa 2010/11, yupo tena ndani ya Listi ya Wachezaji 32 watakaowania Tuzo hiyo kwa Msimu wa 2011/12 pamoja na Cristiano Ronaldo na Xavi Hernández ambao aliwashinda kwenye hatua ya mwisho ya kugombea Tuzo hiyo.
Tuzo hii ilifufuliwa upya na Rais wa UEFA, Michel Platini, na kwa mara ya kwanza alitunukiwa Lionel Messi Mwezi Agosti Mwaka jana.
Mshindi wa Tuzo hii atapewa Tuzo yake hapo Agosti 30 huko Monaco.
Kama ilivyokuwa Mwaka jana, Jopo la Wanahabari toka kila Nchi Wanachama wa UEFA, Nchi 53, itatoa Listi ya Wachezaji wao Bora huku wa kwanza akipewa Pointi 5, wa pili 4 na kuendelea.
Hapo Agosti 14, Listi hiyo itapunguzwa na kubakisha Wachezaji watatu ambao watapigiwa kura ‘laivu’ Agosti 30 na Wanahabari hao hao toka Nchi 53 Wanachama wa UEFA.
Messi ni mmoja wa Wachezaji wanne wa Barcelona ambao wapo kwenye Listi ya Wachezaji 32 na wengine ni Xavi, Andrés Iniesta na Cesc Fàbregas.
Real Madrid inao Wachezaji 6 wakiwemo Xabi Alonso, Iker Casillas na Sergio Ramos.
Manchester City inao Wachezaji 6 na Chelsea, ambao ndio Mabingwa wa Ulaya, wanao Wachezaji wanne.
LISTI KAMILI YA WACHEZAJI 32:
Sergio Agüero (ARG) – Manchester City FC
Xabi Alonso (ESP) – Real Madrid CF
Mario Balotelli (ITA) – Manchester City FC
Jakub Błaszczykowski (POL) – Borussia Dortmund
Gianluigi Buffon (ITA) – Juventus
Iker Casillas (ESP) – Real Madrid CF
Petr Čech (CZE) – Chelsea FC
Fábio Coentrão (POR) – Real Madrid CF
Leslie Davies (WAL) – Bangor City FC
Didier Drogba (CIV) – Chelsea FC (Amehamia Shanghai Shenhua FC)
Cesc Fàbregas (ESP) – FC Barcelona
Falcao (COL) – Club Atlético de Madrid
Joe Hart (ENG) – Manchester City FC
Zlatan Ibrahimović (SWE) – AC Milan
Andrés Iniesta (ESP) – FC Barcelona
Shinji Kagawa (JPN) – Borussia Dortmund (Amehamia Manchester United FC)
Vincent Kompany (BEL) – Manchester City FC
Frank Lampard (ENG) – Chelsea FC
Lionel Messi (ARG) – FC Barcelona
Luka Modrić (CRO) – Tottenham Hotspur FC
Mesut Özil (GER) – Real Madrid CF
Pepe (POR) – Real Madrid CF
Andrea Pirlo (ITA) – Juventus
Sergio Ramos (ESP) – Real Madrid CF
Raúl González (ESP) – FC Schalke 04 (Amehamia Al-Sadd Sports Club)
Cristiano Ronaldo (POR) – Real Madrid CF
Wayne Rooney (ENG) – Manchester United FC
David Silva (ESP) – Manchester City FC
Fernando Torres (ESP) – Chelsea FC
Yaya Touré (CIV) – Manchester City FC
Robin van Persie (NED) – Arsenal FC
Xavi Hernández (ESP) – FC Barcelona

No comments:

Translate