Bi Nasra mohammed
Bi Nasra akiwa na Ndugu zake Hospitali
Mkazi
wa Bunda mkoani Mara, Elisha Makumbati anadaiwa kumfanyia ukatili wa
kupindukia mkewe, Nasra Mohammed (38) kwa kumburuza na gari uvunguni,
umbali wa mita 150 baada ya kutokea kutoelewana kufuatia wivu wa
kimapenzi.
Akizungumza na gazeti hili dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mwanne Daudi, ambaye alishuhudia tukio hilo alisema:
“Mdogo wangu alifanyiwa ukatili wa kutisha na mumewe kwani Februari 2,
mwaka huu mimi na Nasra tulikuwa tunatoka kwenye saluni moja iliyopo
mtaa wa Posta, maeneo ya Bunda.
“Tukiwa njiani ghafla tulimuona
Elisha ambaye ni mumewe akiwa kwenye gari aina ya Nissan Patrol lenye
namba za usajili T 400 BBC na kulisimamisha mbele yetu kisha akamuita
mdogo wangu kwa hasira.
“Nasra alivyoenda akamuuliza mumewe, kwa
nini alitaka kuwagonga, wakaanza kulumbana na kushutumiana kwa wivu wa
kimapenzi,” alisema Mwanne.
Dada huyo wa marehemu aliendelea kusema
huku akitokwa na machozi: “Baada ya kumaliza malumbano yao mimi na Nasra
tulianza kuondoka, ghafla tukashtukia mumewe akiondoa gari kwa kasi na
kumgonga mkewe na kumburuza kwa umbali wa mita 150 kwa mujibu wa kipimo
cha jeshi la polisi lililopima ajali hiyo.
“Wakati akimburuza mdogo
wangu mimi na umati uliokuwa ukishuhudia tulipiga mayowe ya kumtaka
Elisha asimamishe gari lakini aliendelea kuongeza mwendo huku damu
zikitapakaa barabarani mpaka alipokwenda kukutana na tuta ndipo mwili
ukachomoka uvunguni mwa gari.
“Mdogo wangu Nasra wakati akisagika
kwenye lami mimi nilikuwa nikilikimbiza gari hilo kwa nyuma. Nilipofika
eneo alilochomoka nilimkuta askari wa usalama barabarani ameshafika na
tayari alianza kupima ajali hiyo na muda si mrefu lilifika gari la
polisi ‘Difenda’ na kumpakia Nasra na kumpeleka Hospitali ya Bunda,
maarufu kama DDH.
“Alipopimwa aligundulika amevunjika mbavu saba
zilizosababisha kutoboa mapafu, mguu wa kushoto na kupata majeraha
makubwa mgongoni na sikio la kushoto lilikuwa limenyofoka, kutokana na
hali hiyo alihamishiwa Hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza na
kufikishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Dada huyo wa
marehemu alizidi kusema: “Hali ya mdogo wangu iliendelea kuwa mbaya
ambapo Juni 16, mwaka huu, Hospitali ya Bugando ilimpa uhamisho wa
kwenda Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam
ambapo alifikishiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
“Akiwa
Muhimbili madaktari walimtoa nyama za sehemu mbalimbali na kumrudishia
mgongoni baada ya kuona nyama yote ya mgongoni zilitoka na kujikusanya
sehemu ya makalioni.
“Marehemu mdogo wangu aliendelea kuugulia
maumivu ambapo Jumanne iliyopita, saa saba za usiku aliaga dunia na
tumemzika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar,” alisema Mwanne huku
akifuta machozi na akadai mtuhumiwa mpaka sasa yupo huru mitaani.
Juhudi za gazeti hili kuzungumza na mtuhumiwa huyo ziligonga mwamba baada ya simu zake za mkononi kutopatikana hewani.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananilea Nkya amelaani kitendo hicho na kulit
Chanzo global pablishers
No comments:
Post a Comment