Hii ni baada ya makosa kupatikana wakati wa kujumuisha kura kutoka vituo hivyo.
Wakati mgombea wa Urais, Lopez Obrador, alipowasilisha malalamishi yake kuhusu utaratibu wa uchaguzi huo wa Urais mapema wiki hii, hata wafuasi wake sugu hawakutarajia tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali kiasi hicho.
Maafisa hao wametoa amri kura kutoka vituo 143,000 kuhesabiwa tena.
Hatua hiyo inatarajiwa kuwaridhisha wafuasi wa Bw. Lopez, lakini itamsumbua mgombea anayeongoza, Enrique Pena Nieto.
Bw. Pena Nieto, amekuwa na matumaini ya kutangazwa rais wa Mexico katika muda wa siku chache baada ya uchaguzi wa Jumapili.
Hata hivyo madai kuwa chama chake kilinunua kura katika baadhi ya maeneo, yamesababisha kura kuhesabiwa upya.
Akizungumza na BBC Bw Pena Nieto amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa chama chake kilifuata utaratibu unaofaa.
No comments:
Post a Comment