KAGAME CUP: LEO Yanga kutuma salamu kupitia El Salaam Wau?
Jumanne, 17 Julai 2012 07:32
MECHI ZA LEO:
Julai 17 Jumanne
ATLETICO vs APR [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
WAU SALAAM vs YANGA [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]
=====================================
Baada ya kichapo cha Bao 2-0 walichopewa
na Atletico ya Burundi katika Mechi ya ufunguzi ya Kundi C, Mabingwa
watetezi wa Kagame Cup, ambayo ndio Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na
Kati, Yanga leo wataingia tena Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
kucheza na El Salaam Wau ya South Sudan ambayo ilitandikwa Bao 7-0 na
APR ya Rwanda katika Mechi yao ya kwanza.
Bila shaka, baada ya Uchaguzi ndani ya
Klabu yao ambapo Mfadhili Mkuu, Yussuf Manji alichaguliwa kuwa
Mwenyekiti, Yanga wataingia ‘fulu nondo’ ili kuwapa Mashabiki wao raha
na matumaini mapya.
Kabla ya Mechi ya Yanga na El Salaam
Wau, itakuwepo Mechi kati ya Atletico na APR itakayoanza Saa 8 Mchana
hapo hapo Uwanja wa Taifa.
Jana kulikuwa hamna Mechi yeyote ya
Kagame Cup na badala yake ilichezwa Mechi ya Kirafiki kati ya Timu ya
Taifa ya Vijana wa chini ya Miaka 17 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes, na
wenzao wa Rwanda.
Rwanda ilishinda Bao 2-1.
MECHI ZINAZOFUATA:
Jumatano Julai 18
VITA CLUB vs URA [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
PORTS vs SIMBA [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]
FAHAMU: Mashindano ya
Mwaka huu yanashirikisha Vilabu 11 ambazo zimepangwa katika Makundi
matatu yatakayocheza Mtindo wa Ligi na Timu tatu tatu, kutoka Kundi A na
C yenye Timu 4 kila moja, na Timu mbili toka Kundi B, lenye Timu 3,
ndizo zitaingia Robo Fainali itayochezwa kuanzia Julai 23.
KUNDI A
[Timu 3 kwenda Robo Fainali]
Simba
URA [Uganda]
Vita [Congo DR]
Ports [Djibouti]
KUNDI B
[Timu 2 kwenda Robo Fainali]
Azam FC
Mafunzo [Zanzibar]
Tusker [Kenya]
KUNDI C
[Timu 3 kwenda Robo Fainali]
Yanga
APR [Rwanda]
Wau Salaam [Sudan Kusini]
Atletico [Burundi]
RATIBA/MATOKEO:
Julai 14 Jumamosi
APR 7 WAU SALAAM 0
YANGA 0 ATLETICO 2
Julai 15 Jumapili
3 AZAM 1 MAFUNZO 1
4 VITA CLUB 7 PORTS 0
5 SIMBA 0 URA 2
Julai 17 Jumanne
6 ATLETICO vs APR [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
7 WAU SALAAM vs YANGA [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]
Jumatano Julai 18
8 VITA CLUB vs URA [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
9 PORTS vs SIMBA [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]
Julai 19 Alhamisi
10 ATLETICO vs WAU SALAAM [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
11 MAFUNZO vs TUSKER [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]
Julai 20 Ijumaa
12 PORTS vs URA [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
13 YANGA vs APR [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]
Julai 21 Jumamosi
14 AZAM vs TUSKER [Uwanja wa Taifa, Saa 8 Mchana]
15 SIMBA vs VITA CLUB [Uwanja wa Taifa, Saa 10 Jioni]
ROBA FAINALI
Julai 23 Jumapili
16 B2 vs C2
17 A1 vs C3
Julai 24 Jumatatu
18 C1 vs A2
19 B1 vs A3
NUSU FAINALI
Julai 26
20 Mshindi 16 vs Mshindi 17
21 Mshindi 18 vs Mshindi 19
Mshindi wa 3:
Julai 28 Jumamosi
Aliefungwa 20 vs Aliefungwa 21
FAINALI:
Julai 28 Jumamosi
23 Mshindi 20 vs Mshindi 21
No comments:
Post a Comment