tangazo

Monday, July 23, 2012

MAITI NYENGINE TANO ZAOPOLEWA AJALI YA MV SKAGIT ILIYOZAMA JUMAATANO ILIYOPITA.

                     Maiti wa ajali ya mv skagit alieopolewa jana ikiwa imeharibika vibaya sana
                             Maiti wa ajali ya mv skagit alieopolewa jana ikiwa imeharibika vibaya sana

Maiti nyengine tano zimepatikana jana baada ya juhudi  za wazamiaji ambao wako katika eneo ambalo ajali ya mv skagit ilitokea mnamo siku ya jumaatano tarehe 18/07/2012 majira ya saa 7 mchana baada ya kupatwa na dhoruba kali sana.

Kwa mujibu wa wazamiaji hao wamesema kuwa kunamaiti nyingi sana sehemu ya tukio ila kikwazo ambacho kinawafanya washindwe kufanya kazi hiyo ya kuopoa maiti ambazo ziko chini ya bahari ni ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi.

Aidha wazamiaji hao wanailaumu sana serekali kwa kushindwa kuliwekea umakini sana tukio hili ambalo limepoteza watanzania wenzetu zaidi ya 79 ambao hawajilikani wako wapi hadi hivi sasa.
Mmoja wa wazamiaji hao amesema kuwa kuwa maiti zimeharibika sana kiasi cha kushindwa kutambulika baada ya kuanza kuliwa na samaki baadhi ya sehemu zao za mwili hasa zaidi sehemu za machoni na sehemu za siri.

Aidha maiti ambazo zimepatika zilibidi zikazikwe haraka sana kwani zilikuwa zinatoa harufu jambo ambalo ilibidi serekali itoe uamuzi huokwani hazifai hata kupelekwa monchuary(sehemu ya huhifadhia maiti).

                      Natoa pole kwa wafiwa wote ambao wamepoteza ndugu zao katka hii ajali ya kuzama kwa meli ya mv skagit.

No comments:

Translate