Hili ndilo basi la Tony Sley ambalo limepata ajali jana usiku na kuua watu watatu na kujeruhi 38
Majeruhi wakisubiri matibabu Hospitali ya mkoa wa Iringa. Majeruhi wa basi la Tony Sley Bi Agnesy Lukasi akiwa na mtoto wake Dina Lukasi (4) wakisubiri kupewa matibabu katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kufikishwa hapo usiku huu wakitokea eneo la ajali mlima wa Kitonga
Majeruhi wakipatiwa huduma Hospitali ya mkoa wa Iringa
Ajali ya basi ya  Tony Sley yenye namba za usajili T  218 ACH lililokuwa likitokea  Tunduma mkoani Mbeya kwenda  jijini  D’Salaam  imeua   watu  watatu  wakiwemo  wawili  raia ya Zambia na mmoja mtanzania na kujeruhi wengine 38.
Ajali  hiyo  imetokea katika eneo la  kona za mlima wa kitonga kwenye barabara  kuu ya Iringa –D’Salaam  jana majira ya  saa 12  za  jioni  baada ya  dereva wa basi hilo  kushindwa kulipita  lori  lilolokuwa mbele yake.
Wakizungumza katika eneo hilo na Hospitali ya mkoa wa Iringa majeruhi  wa ajali  hiyo  waliolazwa katika  hospitali ya  wilaya ya  Kilolo Ilula  walisema  kuwa  chanzo  cha  ajali hiyo ni  uzembe  wa  dereva   wao alisema  Agnes Lukasi (30).
Agnesy  alisema kuwa  kwa upande wake  alikuwa amekaa siti ya  mbele na  wakati  dereva huyo akifanya uzembe  huyo  walikuwa  wakimshuhudia hata  kujaribu kumuonya  bila mafanikio.
Alisema kuwa  katika  basi hilo  alikuwa na mtoto  wake Dina Lukas (4) ambaye  pia amejeruhiwa  katika paji lake   la uso.
Kamanda  wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa Michael Kamhanda  ambaye  alifika  eneo la  tukio  pamoja na mkuu  wa kikosi cha  usalama barabarani mkoa  wa Iringa  aliuthibitishia  mtandao huu  kuwa  jumla  ya  abiria 38  ndio  waliojeruhiwa katika ajali  hiyo.
Aliwataja  baadhi ya majeruhi  ambao  majina  yao  yamepatikana na  kulazwa katika  hospital teuli ya mkoa  wa Iringa  kuwa
ni pamoja na Boyd Simwings(43) , Violet Chambale(35),Zilombo
Wake(38),Warmen Mambwe (33),Eugen Maluge(39), Mwamba Andrew (27) ,
Bright Mwalukanga (33) na John Lemba( 30) wote  raia wa Zambia.
Wengine  ni  Martine  Shombe( 29) mkazi  wa Tunduma, Zainabu  Amuri (32) mkazi  wa D’Salaam , Efrain Mwampashi (31) mkazi wa Tunduma, Sebastian Mhaya(25) mkazi  wa Tunduma, Vedastus  Benjamin (11) mkazi  wa Tunduma, Mrashi Handu (38) mkazi  wa Igulusi, Juma Ramadhan (40) mkazi wa Tunduma, Twaribu Juhim (39) mkazi wa Arusha, Muka Muka (26) mkazi  wa  Tunduma, Edina Ramadhan (3) mkazi  wa  Tunduma na Benjamin Enock (33) mkazi  wa Mbeya.
Wengine ni Agness Lukas (30) mkazi  wa  Tunduma  , Dina Lukas (4) mkazi  wa  Tunduma Beatrice Msakanti( 42) mkazi wa Zambia, Besa Shadrack (32) mkazi  wa Zambia na Mary Mumba (48) mkazi wa  Zambia pia.
Alisema  majina ya  majeruhi  zaidi  yatapatikana  hivi karibuni baada ya majeruhi  waliopo Hospital ya  wilaya ya  Kilolo Ilula kufika mjini Iringa.
Mbali ya  majeruhi hao  pia  aliwataja  waliopoteza maisha katika ajali  hiyo kuwa ni Cla Pily (32)  na Dany Kawina (43) wote   wafanyabiashara  raia  wa  Zambia  pamoja na Abel Nelson (32) ambaye ni mtanzania.
 
No comments:
Post a Comment