tangazo

Friday, July 6, 2012

TEKNOLOJIA MPYA YA GOAL LINE KUANZA KUTUMIKA LIGI KUU YA UINGEREZA 2012-2013


Teknolojia ya kuthibitisha kama mpira umevuka msitari na kuingia wavuni, inayofahamika kama 'Goal-line technology', huenda ikatumiwa katikati ya msimu wa ligi kuu ya Premier ya England, ya mwaka 2012 hadi 2013, baada ya utaalamu huo kuidhinishwa na halmashauri ya kimataifa ya mchezo wa kandanda, IFAB, Alhamisi, mjini Zurich.



Teknolojia mbili ziliidhinishwa, moja ikifahamika kama 'Hawk-Eye', yaani 'jicho la mwewe', na ya pili inafahamika kama 'GoalRef', ikimaanisha 'mwamuzi wa goli'.



Teknolojia hiyo kwa mara ya kwanza itatumiwa katika michuano ya Kombe la Dunia la vilabu vya soka mwezi Desemba, na iwapo itaonekana inafaa, basi itatumiwa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho mwaka 2013, na vile vile katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.

Mbinu hiyo ya 'jicho la mwewe' inafanya kazi vipi?

Utaalamu huu unategemea kamera sita, zikiangazia kila lango, na kuufuata mpira uwanjani.

Kisha kiufundi, huwa teknolojia inatambua mahali halisi mpira ulipo, kupitia utaalamu unaojulikana kama 'triangulation'.

Ikiwa mpira utavuka msitari wa goli, basi ujumbe kupitia mawimbi ya redio hutumwa moja kwa moja hadi katika saa ya mkononi aliyovalia mwamuzi, kumwarifu kwamba bao limefungwa.

Kama kanuni za FIFA zinavyohitaji, utaratibu mzima hauchukui zaidi ya sekunde moja.

Teknolojia ya 'GoalRef' nayo hutumia kifaa kinachojulikana kama 'microchip', ambacho hubandikwa katika mpira unaotumiwa, na kwa kutumia mawimbi ya smaku karibu na goli.

Iwapo mabadiliko funali yatajitokeza katika mawimbi kupitia mpira kuvuka msitari, teknolojia inaamua kama hilo ni goli, na kisha kwa njia ya elektroniki, mwamuzi hujulishwa katika muda wa sekunde moja kwamba goli limefungwa.

Wasimamizi wa ligi kuu ya Premier wamesema wanataka kuanza kuitumia teknolojia hiyo mpya haraka iwezekanavyo.

Katika mkuu wa chama cha soka cha England, Alex Horne, amesema ni wajibu wa wasimamizi wa ligi kuu ya Premier kuamua ni lini wangelipenda kuanza kuitumia teknolojia hiyo mpya.

"Tayari tuna teknolojia ya Hawk-Eye katika uwanja wa Wembley, kile kinachohitajika tu ni kuiweka sawa na kuhakikisha inafanya kazi vizuri na kuidhinishwa kwa leseni, na kwa hiyo tumekaribia sana kukamilisha matayarisho yetu katika kuitumia teknolojia hiyo.

"Kombe la FA huenda likatufanyia uamuzi, kwa kuwa tunaweza kuitumia katika nusu faianli na fainali za FA, na sidhani huo ni uamuzi ambao utata."

Horne aliongezea kwamba anahisi "hii ni siku muhimu sana" kwa kandanda.

No comments:

Translate