Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wamemsafirisha kutoka Dar es Salaam kumleta ZanzibarMeneja wa Meli ya Skagit Bw Omari Hassan Mnkonje(50) ili kuunganishwa na watuhumiwa wengine wanaohojiwa na Polisi visiwani hapa.
Naibu
Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amesema kuwa meneja
huyo wa ambaye ofisi zake zipo Jijini Dar es Salaam ameunganishwa na
watuhumiwa wengine katika kesi hiyo.Meneja huyo alikuwa akishikiliwa na
Polisi Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo na
kwamba ataunganishwa pamoja na wenzake wengine waliokuwa wakihojiwa na
Polisi Visiwani hapa.
Katika
hatua nyingine Kamanda Ilembo amesema kuwa watuhumiwa watatu kati ya
sita waliokuwa wakihojiwa kuhusiana na tukio hili wamewaachiliwa baada
ya kuonekana kuwa hawahusiki katika tukio hilo.
Waliohojiwa
na kuachiliwa huru ni pamoja na Fundi wa zamu wa meli hiyo Bw. Hamis
Mbarouk Juma(60) ambaye naye alikuwa miongoni mwa manusura katika ajali
hiyo.Wengine walioachiliwa baada ya mahojiano hayo ni Mtaalamu wa Vifaa
katika meli hiyo Bw.
Ahmed
Mashaka Mbarouk(51) mkazi wa Vikokotoni na Mhudumu wa Meli hiyo Bw.
Shaibu Godfrey Francis Kanuti(33), mkazi wa Tombondo mjini
Zanzibar.Watuhumiwa wanaoendelea kushikiliwa na Polisi liobaki katika
kesi hiyo na ambao watafikishwa mahakamani siku za usoni Watuhumiwa hao
watafikishwa mahakamani mara watakapokamilisha masuala ya
mahojiano.Wakati huo huo, Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
wanaoshiriki katika kazi ya utafutaji wa maiti leo wamefanikiwa
kuzipata maiti nyingine watano na kufanya idadi ya maiti zilizopatikana
hadi sasa kufikia 78.
Miongoni
mwa maiti zilizoopolewa leo, moja imetambuliwa kuwa ni Askari wa Jeshi
la Wananchi wa Tanzania JWTZ Kikosi cha Bendi Zanzibar STG Suleiman
Pandu Jape.
Katika
Maiti zilizopatikana leo, nne zilikuwa za wanaume akiwemo mtoto mdogo
na mmoja ni ya mwanamke ambapo kufuatia kuharibika kwa miili hiyo,
Kamishna wa Polisi zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuwa maiti
hizozimefanyiwa mazishi katika makaburi ya pamoja yaliyopo eneo la Kama
nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment