Mawaziri wanaohusika na usafiri baharini Zanzibar, Hamad wa kulia Dk
Harison Mwakyembe na Said Ali Mbarouk waziri wa habari wakitoa taarifa
kuhusiana na ajali ya meli juzi katika ukumbi wa ZBC Zanzibar
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad
amejiuzulu wadhifa wake leo jioni imeelezwa. Kwa mujibu wa taarifa ya
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid
Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.
Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud
kujiuzulu.
“Tarehe 20 Julai,2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano
Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohammed Shein ya kumuomba
ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit iliyotokea
Julai 18,2012” Ilisema taarifa ya Dk. Mzee.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dk Shein amemteua
Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani(CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa
Miundombinu na Mawasiliano.
“Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na
Mawasiliano,Rais amemteua Rashid Seif
Suleiman kuwa Waziri wa
Miundombinu na Mawasiliano” Taarifa ya Ikulu ilisema.
Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano umeanza Julai 23 mwaka huu.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya
kuzama kwa meli ya Mv. Skagit.
Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni
Meja Jenerali S.S. Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla
Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein
Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban
Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.
No comments:
Post a Comment