DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA, KUFUATIA AJALI YA KUZAMA KWA MELI YA MV SKAGIT ILIYOTOKEA TAREHE 18
JULAI, 2012, CHUMBE, ZANZIBAR
Jana tarehe 18 Julai, 2012, majira ya
alasiri kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT katika eneo la Chumbe,
Zanzibar. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea
Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250,
watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9.
Amiri
Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliagiza vyombo vya ulinzi na
usalama vya Serikali ya Muungano yaani JWTZ na
Polisi waanze kazi ya uokoaji mara moja.
Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana
na vyombo vya usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na meli za makampuni
binafsi. Mpaka giza lilipokuwa limeingia
na hivyo kazi ya uokoaji kusitishwa mpaka kutakapokucha tarehe 19 Julai, 2012,
watu 136 walikuwa wameokolewa na
maiti 31 zilikuwa zimepatikana. Aidha, mali zilizokuwa kwenye meli hiyo
hazikuweza kuokolewa.
Kufuatia ajali hiyo, Rais wa Jamhuri
ya Muungano alizungumza na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Alimpa pole kwa ajali iliyotokea hasa kwa
vifo na majeraha waliyopata Watanzania wenzetu na watu wasiokuwa raia wa
Tanzania. Alimuomba afikishe salamu za
rambirambi kwa ndugu zetu waliopotelewa na jamaa zao na kuwapa pole waliopata
majeraha na maumivu maungoni mwao. Rais wa Jamhuri ya Muungano alisema kuwa huu
ni msiba wetu sote na kwamba majonzi yao ni majonzi yake na ya Watanzania
wote. Kwa ndugu zetu waliojeruhiwa tunawaombea
kwa Mwenyezi Mungu awape ahueni na wapone haraka ili waweze kuendelea na
shughuli zao za kujiletea maendeleo na kulijenga taifa letu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wote wa ngazi
mbalimbali kwa uongozi wao thabiti tangu taarifa ya kutokea kwa ajali mpaka
sasa. Aidha, amewapongeza maafisa na
askari wa vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyakazi wa meli binafsi, kwa
juhudi kubwa walizozifanya za uokoaji wa ndugu zetu waliopatwa na maafa haya
makubwa na ya aina yake. Amewataka
waendeleze juhudi hizo leo na siku zijazo.
Rais amewataka wananchi wawe na moyo
wa subira na uvumilivu wakati kazi ya uokoaji inaendelea. Kama ilivyofanyika katika ajali ya MV Spice
Islander miezi 10 iliyopita, uchunguzi wa kina utafanyika kubaini chanzo cha
ajali.
Kutokana na ajali hiyo na msiba huu
mkubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho
Kikwete, ametangaza maombolezo ya taifa ya siku tatu ambapo bendera zitapepea
nusu mlingoti kuanzia leo, tarehe 19 Julai, 2012.
Asanteni
sana.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
19 Julai, 2012
No comments:
Post a Comment