Jamaa wa mmoja wa marehemu wa ajali ya Boti akiwa na simazi ya
kuondokewa na jamaa yake katika tukio la ajali hiyo, baada ya kuitambua
maiti ya jamaa yake iliopelekwa katika viwanja vya maisara.
Wananchi wakiwa katika Ufukwe wa bahari ya Kizingo wakiangalia kama
kutakuwa na miili kuangukia katika ufukwe huo ili kuwatambua jamaa zao.
Wananchi wakikagua maiti ili kutambua maiti za jamaa zao katika viwanja
vya maisara ambavyo vimetengwa kwa ajili kufikisha maiti wanaookolewa
katika ajali hiyo.
Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Zantel wakitowa huduma ya maji na
biskuti kwa Wananchi wanaofika kutambua miili ya jamaa zao na watoa
huduma katika kituo hicho.
Waheshimiwa Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mashehe
wakiwa katika viwanja vya maisara kuwafariji jamaana ndugu waliofiwa na
jamaa zao.
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Hamad Masoud akizungumza na
waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika viwanja vya
maisara kulikotengwa kwa ajili ya kuwatambua marehemu wa ajali ya boti
iliotokea jana 18-7-2012 katika bahari ya Zanzibar maeneo ya Chumbe,
Mmoja wa Abiria aliyenusurika katika ajali hiyo Tatu Piela , akipata
kikombe cha uji kutoka kwa wasamaria waliofika katika viwanja vya
maisara , ambaye na mweji wa Isaka Shinyanga, amepoteza mtoto Said
Jumanne mwenye umri wa miezi 9 wake, akisubiri kukabidhiwa maiyi yake
kwa ajili ya kwenda kuzika.
Jamaa wa Marehemu Sauda Juma ambaye ni Raia wa Ruwanda ambaye ambaye
amafariki katika ajali hiyo, wakisubiri maiti yao ili kwenda kuzikwa.
Rais Mstaaf Mhe Ali Hassan Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa
vyombo mbalimbali waliofika katika eneo hilo maalum kwa ajili ya
kuwatambua maiti wa ajali ya boti.
No comments:
Post a Comment