tangazo

Friday, July 6, 2012

THOMAS ULIMWENGU ANUSURIKA KATIKA AJALI YA NDEGE.

                                                            Thomas Ulimwengu.




MSHAMBULIAJI nyota wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu jana alinusurika kifo katika ajali ya ndege iliyotokea nchini DR Congo.
Ulimwengu raia wa Tanzania anayekipiga TP Mazembe alinusurika katika ajali hiyo akiwa katika ndege iliyokuwa inajaribu kuruka lakini ikashindwa.
Kutokana na kushindwa kupaa, ndege hiyo iliacha njia na kuingia vichakani, Ulimwengu akiwa ndani pamoja na wachezaji wengine 15 wa TP Mazembe na timu ya benchi la ufundi.
Taarifa za ajali hiyo jana zilipatikana saa 8 mchana kupitia katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook wa Ulimwengu ambaye aliweka maneno haya.
“Dakika chache zilizopita kungelewa mambo mengine, labda ningeitwa marehemu au ningekuwa hospitali. Niko ndani ya ndege mimi na wachezaji kama kumi na tano na viongozi na makocha.

Ndege imeacha njia na kuingia vichakani, ni baada ya kushindwa kupaa. Mungu mkubwa.”
Baada ya maneno hayo ya Ulimwengu, watu kadhaa walikuwa wakimpa pole mfululizo huku wakimuombea afya njema.
Championi Ijumaa lilifanya juhudi kumpata ili aweze kufafanua maswali mengi kama ndege hiyo ilikuwa inatokea wapi kwenda wapi na kama alikuwa pamoja mchezaji Mtanzania Mbwana Samatta au la.

No comments:

Translate